Sayyid Swafi awahutubia wahusika wa mradi wa kiongozi wa wasomaji: Saa mnazo tumia kwa ajili ya Qur’an tukufu kwa ikhlasi na nia nzuri zina athari kubwa kweni na zitafungua mambo ya baadae..

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Muheshimiwa Sayyid Ahmad Swafi (d.i) amesisitiza kua: “Hakika saa mnazo tumia kwa ajili ya Qur’an tukufu kwa ikhlasi na nia nzuri ndani ya umri wenu, ni Allah pekee ndiye anaejua ukubwa wa faida yake kwa sababu zitakufungulieni mambo yenu ya baadae, kama alivyo sema Kiongozi wa waumini (a.s) (Hadhi ya kila mtu inatokana na yale anayofanya vizuri)”.

Haya aliyasema katika maelezo elekezi aliyo toa pindi alipo tembelea mradi wa Kiongozi wa wasomi wa kitaifa, unao endelea hivi sasa katika Maahadi ya Qur’an tukufu ndani ya Atabatu Abbasiyya, na akakutana na washiriki pamoja na maustadhi wanao endesha mradi huo, aliongeza kusema kua: “Hakika unufaikaji wenu wa muda katika jambo hili ni mkubwa mno, ubora zaidi ni kwamba faida ya sekunde, dakika na saa unazo tumia ni endelevu milele na milele, hongereni sana kwa nafasi kubwa mliyo nayo kutokana na kufanya jambo hili tukufu, tofauti na wale wanao tumia muda katika mambo yasiyo kua na manufaa kwao, pia ni matarajio yetu kua mtafanya vizuri katika masomo ya kisekula, ili ufaulu wenu uwe katika masomo ya Qur’an na ya kisekula”.

Kisha akabainisha kua: “Atabatu Abbasiyya tukufu ilianzisha Maahadi hii –Maahadi ya Qur’an tukufu- kutokana na kuona umuhimu wa Qur’an, Alhamdu lilaahi; matunda yake yanaonekana, kila mtu anayashuhudiwa tena kwa kuthibitishwa na wataalamu wa nje kabla ya kuthibitishwa na watu wa Ataba wenyewe”.

Akamalizia maneno yake kwa kuushukuru uongozi wa Ataba tukufu kwa kufanya mradi huu na mingine mingi miongoni mwa miradi ya Qur’an, na kuhakikisha wanaondoa kila jambo linalo weza kukwamisha ukamilifu wa mradi huu, hali kadhalika akatoa shukrani kwa watumishi wa jengo la Alqamiy lililo chini ya Ataba tukufu, ambalo mradi huu unafanyika ndani ya jengo hilo kwa mwaka wa pili mfululizo sasa, pamoja na viongozi wa Maahadi kwa usimamizi mzuri katika utekelezaji wa mradi huu mtukufu”.

Kiongozi mkuu wa kisheria katika ziara hii aliongozana na katibu mkuu wa Ataba tukufu Muhandisi Muhammad Ashiqar (d.t) pamoja na wajumbe wa kamati kuu ya uongozi na marais wa vitengo, bila kumsahau mkuu wa Maahadi ya Qur’an tukufu Shekh Jawaad Nasrawiy na mkuu wa miradi ya Qur’an Sayyid Hasanain Halo pamoja na mkuu wa utekelezaji wa mradi Ustadh Ali Bayatiy, ziara hii ilihusisha kutembelea kumbi za masomo na kusikiliza zana zinazo tumiwa katika mradi.

Kumbuka kua mradi wa Kiongozi wa wasomaji wa kitaifa, unalenga kujenga kizazi kinacho jitambua na kushikamana na mafundisho ya Qur’an tukufu katika maisha yao, pamoja na kulea vipaji vya usomaji wa Qur’an kwa watoto kupitia masomo ya muda mfupi kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari (upili) kutoka katika mikoa yote ya Iraq. Na kuhakikisha tunatumia vizuri muda wa likizo za kiangazi kwa kuandaa kundi kubwa la wasomaji, na kuhakikisha wanakua na kiwango kizuri cha usomaji wa Qur’an katika kipindi cha miezi miwili takriban katika hatua ya kwanza ya mradi huu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: