Wakfu shia wagawa zawadi kwa washindi wa mashindano ya Qur’an ya kimataifa kwa wahitimu wa kituo cha miradi ya Qur’an na rais wake asifia mafanikio haya..

Maoni katika picha
Kutokana na kuonyesha thamani ya mafanikio yaliyo fikiwa katika mashindano ya Qur’an ya kimataifa, uongozi mkuu wa wakfu shia wamegawa zawadi kwa washindi walio wakilisha Iraq katika mashindano hayo na kupata nafasi za kwanza, miongoni mwao kuna wahitimu wa kituo cha miradi ya Qur’an kilicho chini ya Maahadi ya Qur’an tukufu katika Atabatu Abbasiyya.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na rais wa wakfu shia Muheshimiwa Sayyid Alaa Mussawiy, na wawakilishi wa Ataba tukufu pamoja na kundi la wadau wa Qur’an na jopo la viongozi wa wakfu shia.

Mkuu wa kituo cha kitaifa cha maarifa ya Qur’an dokta Raafi Al-aamiriy alisema kua Iraq ilikua haijapata nafasi za juu katika mashindano haya tangu miaka mitano iliyopita, jambo hilo ndio lililo pelekea kituo cha maarifa ya Qur’an cha kitaifa kuanza kulea vijana wenye vipaji na vipawa vya Qur’an katika sekta mbalimbali na kufanya mashindano ya kitaifa halafu wale wanaoshinda katika mashindano hayo ndio wanachaguliwa kwenda kuwakilisha taifa katika mashindano ya kimataifa.

Rais wa wakfu shia akaonyesha umuhimu wa Qur’an tukufu na ulazima wa kufuata mafundisho yake “Hakika kupatikana kwa kundi hili la vijana hapa Iraq kunatia moyo, na akatoa shukrani kwa watumishi wote wa kituo cha maarifa ya Qur’an na akawaombea kwa Mwenyezi Mungu aendelee kuwapa uwezo wa kulea watu hawa muhimu”.

Mwisho wa hafla hiyo washindi wa mashindano ya kimataifa wakapewa zawadi pamoja na vyeti vya heshima pia walimu wao nao wakapewa zawadi kwa kazi kubwa waliyo fanya ya kuibua na kulea vipaji vya vijana hoa.

Miongoni mwa walio pewa zawadi ni mkuu wa utekelezaji wa mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa Ustadh Ali Bayati na baadhi ya vijana walio hitimu katika mradi wa kitaifa wa kuandaa wasomi na mahafidh wa Qur’an hapa Iraq unao fanywa na kituo cha miradi ya Qur’an ambao ni:

Mshindi wa kwanza katika shindano la kimataifa (Inna lilmutaqina mafaazaa) msomaji Leeth Abedi.

Mshindi wa pili katika shindano la 34 katika Jamhuri ya kiislamu ya Iran, msomaji Falaah Zaleef.

Mshindi wa tatu wa hifdhu katika shindano la kimataifa katika Jamhuri ya kiislamu Iran, Haafidh Hussein Ghazi.

Mshindi wa tatu katika shindano la kimataifa la usomaji katika Jamhuri ya kiislamu ya Iran, Msomaji Muhammad Abdu-shaheed.

Mshindi wa sita katika shindano la kimataifa la wanafunzi wa shule za wenye vipaji, Zainul-abidina Abbasi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: