Ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu wahudhuria hafla ya ufunguzi wa kongamano la mwaka la mashairi ya kiarabu..

Maoni katika picha
Ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu ukiongozwa na katibu wake mkuu Muhandisi Muhammad Ashiqar (d.t) umehudhuria ufunguzi wa kongamano la kumi na sita kuhusu mashairi ya kiarabu linalo fanyika katika Atabatu Kadhimiyya tukufu.

Kongamano la mwaka huu limeanza jioni ya siku ya Alkhamisi (17 Dhulqa’adah 1438h) sawa na (10 Agosti 2017m) ndani ya ukumbi mtukufu wa haram ya Imamu Kadhim (a.s), chini ya kauli mbiu isemayo: (Nafasi ya mashairi katika kuelekea mustaqbali bora), hafla hiyo ilipata mahudhurio makubwa ya wawakilishi wa Ataba tofauti na Mazaru tukufu, na idadi kubwa ya watu muhimu kidini, kijamii na kisiasa pamoja na watumishi wa maimamu wawili watakatifu (Jawaadaini) (a.s), na jopo la washairi, waandishi na watalamu wa mashairi faswaha ya lugha ya kiarabu.

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukifu, kisha ukafuata ujumbe wa Atabatu Kadhimiyya, ulio wasilishwa na katibu mkuu wa Ataba hiyo, miongoni mwa aliyo sema ni: “Hakika kongamano hili ambalo tumehudhuria, linavionjo zaidi kushinda makongamano yaliyo pita kwa kukaribisha lugha ya kitalamu ya kimashairi, kwa ajili ya kueneza utamaduni wa mabadiliko na maelewano katika jamii, na kuhakikisha tunatengeneza mustaqbali mwema, na kutoa malezi sahihi, kuhimiza kupambika na lugha nzuri za kimashairi ya Amudi, na kupambana na uporaji wa alama za kiislamu pamoja na vita ya kitamaduni inayo lenga kuharibu mashairi ya kiislamu na kupoteza uzuri wake”.

Kisha washairi wakaanza kuingia ulingoni, ukumbi ukapambwa kwa sauti murua za mashairi mazuri mazuri, zikasikika beti nzuri za mashairi ya kitalamu zilizo somwa na washairi hao watukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: