Kwa mara ya kwanza hapa Iraq na katika hospitali ya rufaa Alkafeel wafanyika upasuaji wa kuweka kiungo cha kutengenezwa..

Maoni katika picha
Mfululizo wa pasuaji zenye mafanikio na ambazo ni nadra kufanywa, kiongozi mkuu wa hospitali ya rufaa Alkafeel Dokta Haidari Bahadeli ametangaza mafanikio ya jopo la madaktari wa kihindi wanao fanya kazi katika hospitali hiyo ya kuweka kiungo mbadala kwa mgonjwa.

Jopo la madaktari walifanikiwa kumuwekea kiungo mbadala mgonjwa kutoka Bagdad kwa kutumia njia ya kisasa kabisa, njia hii imetumika kwa mara ya kwanza hapa Iraq, baada ya kua ilikua inatumika katika hospitali za kimataifa nje ya nchi, jambo hili ni mafanikio makubwa sana katika sekta ya matibabu hapa nchini.

Akaoneza kusema kua: “Mgonjwa alikua na maumivu makali kufuatia ajali aliyo pata ya kuanguka, baada ya kufanyiwa vipimo na uchunguzi wa kina, pamoja na ukubwa wa umri wake, ambapo anamiaka (63) lakini wataalamu wetu walionyesha uwezekano wa kufaulu kwa kumfanyia upasuaji na kumbadilisha kiungo kilicho haribika, kutokana na vifaa tiba vya kisasa vinavyo milikiwa na hospitaji, pamoja na uwezekano wa kuagiza viungo vya kuundwa vya kisasa zaidi, vinavyo tofautiana kabisa na (double mobility), viliagizwa viungo vya kisasa kutoka ufaransa vinavyo weza kutumika katika zoezi hili”.

Akasisitiza kua: “Hakika aina hii ya viungo vya kutengeneza inamlinda mtu na athari mbaya inayo weza kupatikana kutokana na baadhi ya aina za ukaaji wa juu ya aridhi, kwa matibabu haya tunaweza kusema kua hospitali imeingia katika ubora wa kimataifa, hakuna haja tena ya wagonjwa kusafiri kwenda nchi za nje, hospitali ya rufaa Alkafeel imekua na uwezo mkubwa wa kufanya upasuaji na matibabu makubwa kama haya kwa raia na wageni”.

Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma zinazo tolewa na hospitali ya rufaa Alkafeel unaweza kutembelea toghuti yetu ifuatayo: www.kh.iq au piga namba zifuatazo: (07602344444 au 07602329999).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: