Makumbusho ya Alkafeel yaongeza uwezo wa watumishi wake kwa kuwapa semina ya kutengeneza miswala..

Maoni katika picha
Makumbusho ya Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya tukufu inawapa semina ya kutengeneza miswala watumishi wake, semina hii ni miongoni mwa semina nyingi ambazo hulenga kuongeza ujuzi wa watumishi katika mambo mbalimbali, na kuwafanya watambue mambo yote yanayo husiana na utunzaji wa makumbusho, semina hii itadumu mwezi mzima kisha itafuatiwa na semina zingine.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha makumbusho Ustadh Swaadiq Laazim alisema kua: “Tuna semina mfululizo, kutokana na ratiba iliyo pangwa na kitengo hiki kwa kushirikiana na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, hii ni semina ya kumi, inahusu utengenezaji na utunzaji wa miswala, mkufunzi wa semina hii ni mtaalamu Masudi Haidari mtu aliye bobea katika utengenezaji wa miswala na utunzaji wake, anafanya kazi katika makumbusho ta taifa kitengo cha miswala huko Tehran, tulikubaliana naye tangu miaka mitatu ya nyumba kuhusu kuwafundisha watumishi wetu wa makumbusho ya Alkafeel utunzaji wa miswala”.

Akaongeza kusema kua: “Hivi sasa wamepiga hatua kubwa katika utengenezaji wa miswala, mtaalamu huyo amewasifu watumishi kwa utengenezaji na utunzaji wa miswala, kama unavyo fahamu ulimwengu wa kutengeneza miswala ni mpana sana, hali kadhalika wametengeneza kitambaa na baadhi ya vipande vya miswala ambavyo ni miongoni mwa kazi za mikono, pia tuna mradi wa kuwafundisha kutengeneza miswala kwa mikono na sasa hivi tumeanza kuwaonyesha mfano wa kazi hiyo, ambayo ni miongoni mwa mipango muhimu ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Fahamu kua ujuzi walio nao watumishi wa kitengo cha makumbusho wameupata kutokana na uzoefu wao wa kazi, wakati wa nyuma walipata semina maalumu kutoka kwa mmoja wa watumishi wa makumbusho ya Iraq (taifa) kwa muda wa siku kumi na tano, iliyo husu namna ya utunzaji bora wa miswala, semina hiyo ilifanyika chini ya makubaliano ya kusaidiana baina ya makumbusho na kubadilishana uzoefu wa kazi, semina hiyo ilifanyika baada ya watumishi wa makumbusho ya Alkafeel kutunza mswala wa kihistoria wa makumbusho ya Iraq (taifa), pamoja na kutoa waraka wa maelezo kuhusu mswala huo haya yote yanafanyika chini ya makubaliano yaliopo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: