Kikosi cha zima moto chini ya kitengo cha usimamizi wa kihandisi chafunga vifaa vya kuzima moto moja kwa moja (Automatic) katika Maahadi ya Alkafeel ya kutoa elimu na kukuza vipaji..

Maoni katika picha
Kikosi cha zima moto kimefunga mitanbo ya kuzima moto moja kwa moja (Automatic) katika jengo la redio ya Alkafeel ya wanawake na Maahadi ya Alkafeel ya kutoa elimu na kukuza vipaji zilizo chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kiongozi wa kikosi cha zima moto Muhandisi Haidari Jawaad Kaadhim ameelezea kuhusu ufungaji wa mitambo hiyo kua: “Katika hatua ya kwanza ya ufungaji wa mitambo hii wataalam wetu walichora michoro iliyo onyesha sehemu za kupitisha bomba zanazo beba gesi ya (tow carbon assid) na nyaya pamoja na sehemu za kufunga mitambo ya kubaini mioshi na moto inayo onganishwa na mtambo mkuu, ili kuhakikisha kazi inafanyika katika ufanisi na ustadi mkubwa sawa na mashirika makubwa ya kimataifa”.

Akabainisha kua: “Mtambo huu hutoa gesi ya (tow carbon assid) ambayo huteketeza (oxygen) pindi moto unapo waka, gesi hiyo ina ubaridi mkali sana unao elekea katika barafu, husaidia kupoza kwa haraka sememu iliyo ungua, inapo tokea dalili ya moto mitambo hulia alam ya tahadhari, na moto unapo waka, mitamo hutoa gesi na kwenda kuuzima moto huo, gesi hiyo ni rafiki wa vifaa vya umeme kwani huenda moja kwa moja sehemu inayo waka bila kuathiri sehemu zingine”.

Akafafanua kua: “Kutokana na juhudi binafsi za watumishi wa Ataba tukufu kazi hii imefanyika kwa nusu ya gharama ambazo hutozwa na mashirika yanayo fanya kazi hii, jambo hili limesaidia kupunguza matumizi ya Ataba, hili jambo ni muhimu sana kimaendeleo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: