Hivi punde: Majemedari wa kikosi cha Abbasi waanza kutekeleza jukumu walilopewa katika vita ya kukomboa mji wa Tal-afar..

Maoni katika picha
Wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s) pamoja na wa vikosi vya jeshi la serikali na vikosi vingine vya Hashdi Sha’aba, asubuhi ya leo wameanza kusonga mbele katika vita ya kukomboa mji wa Tal-afar, chini ya maelekezo ya viongozi wakuu wa jeshi huku wakiwa na hamasa kubwa kabisa.

Kumbuka kua asubuhi ya leo (Juma Pili 27 Dhulqa’adah 1438h) sawa na (20 Agosti 2017m), imeanza rasmi vita ya kuukomboa mji wa Tal-afar ngome ya mwisho ya magaidi wa Daesh katika mji wa Mosul.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: