Maendeleo ya haraka yashuhudiwa katika upanuzi wa Maqaamu ya Imamu Mahdi (a.f)..

Maoni katika picha
Mradi wa upanuzi wa Maqaamu ya Imamu Mahdi (a.f) unaendelea vizuri, kwa kufuata muda uliopangwa na kwa mujibu wa michoro ya kihandisi, hivi karibuni umwagaji zege katika sehemu ya paa la ukumbi wa wanawake wenye ukubwa wa mita (490) na urefu wa mita 6 umekamilika.

Kazi hii imefanyika sambamba na ujenzi wa paa zingine katika mradi huu, paa ya ukumbi wa wanaume yenye ukubwa wa mita (310) na paa ya sehemu ya watumishi yenye ukubwa wa mita (150).

Baada ya kumaliza kazi hizo tutahamia katika matengenezo ya mwisho ya sehemu ya kwanza kwa kuweka madirisha na vinginevyo.

Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu amethibitisha kua: “Shirika linalo tekeleza mradi huu, ambalo ni Shirika la ujenzi la aridhi takatifu chini ya usimamizi wa moja kwa moja kutoka katika kitengo chetu, wanafanya juhudi kubwa kuhakikisha wanamaliza hatua moja baada ya nyingine na hatimae kukamilisha mradi wote kwa ustadi na ubora mkubwa utakao endana na hadhi ya sehemu hii tukufu”.

Kumbuka kua Maqaamu ya imamu Mahdi (a.f) ipo upande wa kushoto wa mto wa Husseiniyya wa sasa unapo ingia katika mji wa Karbala, katika barabara inayo elekea Maqaamu ya Imamu Jafari Swadiq (a.s) ni sehemu (mazaru) mashuhuri. Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya marekebisho katika Maqaamu hiyo, marekebisho hayo yalianzia kwenye kubba hadi katika paa za haramu na maeneo mengine, kutokana na mahala ilipo Maqaamu hii kua haiwezekani kufanyiwa upanuzi katika pande zake tatu, Ataba tukufu imeamua kuifanyia upanuzi katika upande wa mto Husseiniyya ambao ni upande wake wa magharibi, kwa kutumia nguzo za zege na juu yake kuwekwa daraja bila kuzuia au kubadilisha hata kidogo muelekeo wa maji, eneo lililo ongezeka linafikia mita za mraba (1200).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: