Tarehe mosi Dhulhijjah zakutanishwa bahari mbili.. ndoa ya Nuru kwa Nuru..

Maoni katika picha
Katika siku ya kwanza ya mwezi wa Dhulhijjah mwaka wa (2 hijiriyya) ambayo ni siku kama ya leo (1 Dhulhijja 1438h) sawa na (24 Agosti 2017m), ilifanyika ndoa tukufu ya Imamu Ali na bibi Fatuma Zaharaa (a.s) na ikaitwa ni ndoa ya Nuru mbili, tukio hilo hupewa umuhimu mkubwa sana kwa sababu ni ndoa ya watu muhimu na bora zaidi baada ya Mtume (s.a.w.w), na matunda ya ndoa hiyo ni kupatikana kwa maimamu watakasifu wa nyumba ya Mtume (a.s), hali kadhalika ndoa hiyo inaonyesha hadhi ya Imamu Ali (a.s) kwa mtume (s.a.w.w), kwani alimkubalia kumuoa binti yake.

Imekuja kaja katika hadithi iliyo pokelewa na Kashfu Ghummah ya kwamba, maswahaba wengi walijitokeza kumposa bibi Fatuma (a.s) wakakataliwa, lakini alipo jitokeza kiongozi wa waumini Ali (a.s), Mtume alifurahi sana, akasema: Hakuna mtu ambaye ni saizi ya Fatuma zaidi ya Ali.

Alimkubali kwa mahari ndogo sana, na harusi ya kawaida, yote hayo yalifanyika kwa amri ya Mwenyezi Mungu mtukufu, ikafanyika ndoa ya Nuru ikienda kwa Nuru, wanandoa wakaungana; bibi Fatuma na mumewa Ali bun Abutwalib (a.s), ikawa ni nyumba yenye nuru ya Mwenyezi Mungu, iliyo kuja kuangazia uislamu na Qur’an, baada ya Mtume (s.a.w.w) kukamilisha dini na neema kwa waislamu, na Mwenyezi Mungu kuridhia uislamu kua ni dini ya walimwengu. Kutoka kwa Khabaab bun Arti anasema: Hakika mwenyezi Mungu alimuambia Jibril: Muozesheni Nuru kwa Nuru, hivyo walii alikua ni Mwenyezi Mungu, na mshenga ni Jibril, na mwenye kunadi ni Mikael, na mlinganiaji ni Israfil, na mtangazaji ni Izrael, na mashahidi ni malaika wa mbinguni na aridhini, kisha Mwenyezi Mungu akauambia mti wa Tuba: toa ulicho nacho. Ukatoa Duri nyeupe, Yaquti nyekundu, Zabrajad ya kijani na lulu. Ilipo fika siku ya harusi, Mtume (s.a.w.w) akaja na mnyama (farasi) wake, akamwambia bibi fatuma panda! Akamuamuru Salmaan amuongoze huku mtume anamuendesha, walipo kua njiani mtume (s.a.w.w) akasikia sauti, mara akamuona Jibril akiwa na malaika elfu sabini, na Mikael pia akiwa na malaika elfu sabini, Mtume (s.a.w.w) akawauliza, kwa sababu gani mmekuja aridhini? Wakasema: Tumekuja kumsindikiza Fatuma kwa Ali bun Abutwalib, Jibril, Mikael na malaika wote wakapiga takbira, na Mtume Muhammad (s.a.w.w) naye akapiga takbira, zikasikika takpira nyingi za kusherehekea harusi katika usiku huo.

Hivi ndio alivyotaka Mwenyezi Mungu mtukufu, kiendelee kizazi cha Mtume (s.a.w.w) kupitia kwa bibi Fatuma (a.s), matunda ya ndoa hii tukufu yalikua ni kupatukana kwa watoto watano, ambao ni maimamu wawili watakasifu, Hassan Almujtaba na Sayyid Shuhadaa Abuu Abdillahi Hussein (a.s), na mabinti wawili ambao ni Aqilah bani Hashim Zainabu Kubra na Ummu Kulthum (a.s) walizaliwa wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.w), na mtoto wa mwisho ni Muhsin (a.s) aliye uawa kishahidi akiwa tumboni kwa mama yake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: