Semina hii ilikua ni sehemu ya kukamilisha semina zilizo pita, ilikua na maudhui nyindi zinazo muongezea mwalimu maarifa zaidi, na kumfanya kua na uweledi zaidi katika ufundishaji hasa unaoendana na maendeleo ya teknolojia za kisasa na kumfanya aeleweke kwa urahisi zaidi kwa wanafunzi pindi anapo fundisha, washiriki wamethibitisha kua semina hii inamatokeo chanya katika shuguli zao.
Miongoni mwa waliyo someshwa ni:
- 1- Kuunganisha vitendo.
- 2- Kusoma kwa vitendo.
- 3- Kutumia zana mpya katika kufundisha.
- 4- Njia za kisasa za ufundishaji.
- 5- Mihadhara ya ki-itikadi.
Washiriki walisifu na kuishukuru sana Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kuwapa semina hizi zinazo wasaidia sana katika utekelezaji wa majukumu yao ya ufundishaji, na kuwawezesha kutambua mbunu na zana za kisasa katika sekta hiyo jambo ambalo lina manufaa makubwa kwa maendeleo ya taaluma hapa Iraq.