Sayyid Swafi awasili katika uwanja wa vita ya Tal-afar na azungumza na wapiganaji na kuwapa salamu za Marjaa dini mkuu na kupongeza mafanikio yao..

Maoni katika picha
Mwakilishi wa Marjaa dini mkuu ambaye pia ni kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu, Muheshimiwa Sayyid Ahmad Swafi (d.i), amewasilisha salamu za Marjaa dini mkuu Sayyid Ali Hussein Sistani (d.dh) kwa wapiganaji wote wa jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi, na akapongeza mafanikio yaliyo patikana katika vita ya Tal-afar dhidi ya magaidi wa Daesh.

Kufuatia ziara aliyo fanya na kukutana na jopo la viongozi wa wapiganaji wakitanguliwa na kikosi cha Abbasi (a.s) pamoja na kikosi cha Imamu Ali na kile cha Ali Akbar pamoja na viongozi wa vikosi vya jeshi la serikali.

Alipewa maelezo ya kina kutoka kwa viongozi hao kuhusu mafanikio yaliyo patikana katika vita ya kukomboa mji wa Tal-afar ndani ya siku tano tangu kuanza vita hiyo, hakika vikosi vyote vinavyo shiriki katika vita hii vimeonyesha uzalendo na ushujaa wa hali ya juu kabisa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: