Atabatu Abbasiyya tukufu yajipanga kuimarisha ulinzi na usalama katika siku ya Arafa na sikukuu tukufu ya Iddul-Adhha..

Ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)
Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wajipanga kutekeleza mpango wa kuimarisha usalama katika Atabatu Abbasiyya tukufu katika siku ya Arafa na Iddul-Adhha, ambayo imekuja sambamba na usiku wa Ijumaa, kawaida usiku huo; hua na ongezeko kubwa la mazuwaru, ambao huja kutoka kila sehemu ya Iraq na nje ya nchi, kutokana na kuimarika kwa usalama idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka zaidi.

Umewekwa mpango maalumu wa kuhakikisha mazuwaru wanatembea kwa amani na kufanya ibada kwa utulivu huku mazingira yakiwawezesha kufanya ibara kwa wepesi na utulivu, hili ndio lengo la kila mtumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kuhakikisha mazuwaru watukufu wanafanya ibada kwa amani na utulivu wakati wote hususan katika ziara hii tukufu ambayo inahudhuriwa na watu wengi zaidi, watu wameanza kufurika katika eneo hili takatifu tangu asubuhi ya leo Alkhamisi.

Tayali kila kitengo kimepewa majukumu maalumu, kuna wanao tekeleza majukumu yao ndani ya ukumbi wa haram tukufu na wengine nje ya ukumbi, mahitaji muhimu ya kibinadamu yote yameandaliwa, ili kuhakikisha zaairu anamaliza siku yake kwa amani na utulivu katika sehemu hii takatifu.

Kumbuka kua miongoni mwa ziara ambazo huhudhuriwa na mamilioni ya watu ni hii ya siku ya Arafa na sikukuu ya Iddul-Adhha, waumini huja kumzuru imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika siku ya Arafa na usiku wa Iddi pamoja na mchana wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: