Maahadi ya Qur’an tukufu katika Atabatu Abbasiyya inaendelea na kufanya nadwa kuhusu Qur’an..

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’an tukufu inaendelea kufanya nadwa za kielimu kuhusu Qur’an tukufu katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ile iliyo fanywa na tawi la Maahadi hii katika wilaya ya Hindiyya mkoa wa Karbala, iliyo kua na anuani isemayo (Visomo vya Qur’an) ambayo ilizungumzia Qur’an kwa ujumla na riwaya za Ahlulbait (a.s) kuhusu visomo vya Qur’an, dokta Ali Abdulfataah Alhasanawiy ambaye ni mkuu wa kitivo cha masomo ya Qur’an katika chuo kikuu cha Baabil alikua ndio muhadhiri wa nadwa hiyo, pia ilihudhuriwa na mkuu wa Maahadi ya Qur’an tukufu Shekh Jawaad Nasrawiy pamoja na wadau wa Qur’an tukufu na viongozi wa kidini, kisiasa na kijamii kutoka ndani na nje ya wilaya hiyo.

Dokta Hasanawiy katika hotuba yake amezungumzia kuhusu kughafirika kwa wasomaji wa visomo vya Qur’an kunako riwaya za maimamu wa Ahlulbait (a.s), masomo yeyote ambayo hayana athari za Ahlulbait ujue yamefanyiwa hiyana, pia akaelezea baadhi za riwaya za Ahlulbait (a.s) kuhusu visomo vya Qur’an tukufu.

Washiriki waliuliza maswali ambayo yalijibiwa na dokta Abdulfataah Hasanawiy, na akatoa ufafanuzi zaidi katika mambo yaliyo hitaji kufafanuliwa.

Kumbuka kua Maahadi ya Qur’an tukufu imezipa nafasi kubwa nadwa za kielimu kuhusu Qur’an tukufu na huwaalika wasomi wakubwa na watafiti wa mambo yanayo husu Qur’an katika nadwa zake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: