Rais wa kitengo cha makumbusho: Kufungua uhusiano na taasisi za makumbusho za kitaifa na kimataifa pamoja na kusaidiana na kubadilishana uzoefu, ni moja ya matunda ya kongamoano la Alkafeel..

Maoni katika picha
Rais wa kitengo cha makumbusho katika Atabatu Abbasiyya tukufu amesema kua: “Hakika miongoni mwa faida za kongamano hili ni kujenga uhusiano mzuri na taasisi za makumbusho mbalimbali, za kitaifa na kimataifa na kuweka misingi ya kusaidiana na kubadilishana uzoefu, pia linatupa nafasi ya kushiriki katika makongamano tofauti ya makumbusho ya kimataifa na kitaifa yatakayo fanyika sehemu mbalimbali Duniani, pamoja na kuchangia kuanzishwa kwa taasisi za makumbusho hapa Iraq na kusaidia ujenzi wa nyumba za makumbusho ili kuhakikisha zinakidhi vigezo vya kimataifa”.

Hayo yalisemwa na Ustadh Swadiq Laazim rais wa kitengo cha makumbusho ya Alkafeel kwa niaba ya kamati ya maandalizi ya kongamano hili lililo anza siku ya Alkhamisi (15 Dhulhijjah 1438h) sawa na (7 Septemba 2017m).

Aliongeza kusema kua: “Baada ya mafanikio ya kongamano la kwanza la Alkafeel la kimataifa, tulikusudia kufanya kongamano lingine: Kongamano la pili la kimataifa Alkafeel chini ya anuani isemayo (Makumbusho ni mazingira na uchumi), tulianza maandalizi mapema, tukitumia uzoefu tulio pata katika kongamano la kwanza kwa kufanya mazuri tuliyo fanya katika kongamano hilo na kurekebisha makosa yaliyo tokea”.

Imepita karibu miaka miwili tangu kufanyika kwa kongamano la kwanza, akabainisha kua: “Watumishi wetu wa makumbusho wamekua na uwezo mkubwa zaidi katika sekta hii, kutokana na kushiriki kwao katika semina mbalimbali kuhusu mambo ya makumbusho ikiwa ni pamoja na utunzaji na ukarabati wa miswala ya aina zote, ikiwemo ustadi wa upangiliaji wa vifaa kale vya makumbusho wa kisasa”.

Kwa kua miongoni mwa malengo ya kongamano ni kujuana na maprofesa pamoja na wataalamu wa mambo ya kale, ili kuboresha sekta ya makumbusho hapa Iraq, tulifungua milango kwa wataalamu wote, na kupokea tafiti mbalimbali kuhusu mambo ya makumbusho, mikhtasari ya tafiti tulizo pokea imefika (63), mikhtasari hiyo iliwasilishwa kwenye jopo la wataalamu ili ichaguliwe iliyo bora zaidi, nao walichagua mikhtasari (45) na katika hiyo; ikachakuliwa ishirini itakayo wasilishwa katika kongamano hili ili faida iwafikie watu wote walioshiriki kwenye kongamano”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: