Tarehe kumi na nane ya mwezi wa Dhulhijjah, wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) hupokea kwa furaha tukio la sikukuu kubwa ya Iddul-Ghadiir, hili ni tukio tukufu sana, kufuatia tukio hilo tukufu, waislamu huhuisha mapenzi yao na utii kwa kiongozi wa ubinadamu na waumini Ali bun Abuutwalib (a.s), ambaye amekua kiongozi wa kila mu-umin kuanzia siku aliyo shikwa mkono na Mtume (s.a.w.w) na kuunyanyua juu halafu akamtangaza kua ni kiongozi wa waislamu.
Kutokana na tukio hilo, na kufuatia utaratibu uliowekwa na Atabatu Abbasiyya wa kuhuisha tukio hilo tukufu, haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imepambwa vizuri na kuwekwa vitambaa vilivyo dariziwa vizuri na kufungwa taa zenye rangi nzuri inayo ingiza furaha nyoyoni mwa waumini, pia yamewekwa maua katika milango na eneo lote linalo zunguka haram tukufu.
Hali kadhalika, korido za upande wa nje zimepambwa vizuri sana.
Kumbuka kua Iddul-Ghadiir ni siku muhimu sana kwa waislamu ambao ni wafuasi wa Ahlulbait (a.s), katika siku kama hii (18 Dhulhijjah) Mtume (s.a.w.w) alitoa khutuba ndefu na akamtangaza Ali (a.s) kua imamu, khalifa na wasii wake na ndiye kiongozi wa waislamu baada yake, tukio hilo lilifanyika wakati waislamu wanarudi kutoka katika hijja ya kuaga (wadaai) ambayo ni hijja ya mwisho ya Mtume (s.a.w.w) katika sehemu iitwayo Ghadiir Khum, mwaka wa kumi hijiriyya.