Kongamano la kimataifa la Ameed lakamilika, na washiriki wasifu mada za amani na utamaduni..

Maoni katika picha
Kwa kuhudhuria kiongozi wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Msheshimiwa Sayyid Ahmad Swafi na katibu mkuu Muhandisi Muhammad Ashiqar pamoja na kundi kubwa la wasomi na watafiti wawakilishi wa nchi nane pamoja na mwenyeji wao Iraq, alasiri ya siku ya Ijumaa (23 Dhulhijjah 1438h) sawa na (15/09/2017m), kongamano la kimataifa la Ameed lililo kua na mada za: (Amani na utamaduni) lilikamilisha ratiba yake iliyo dumu kwa muda wa siku mbili.

Baada ya kusomwa Qur’an tukufu dokta Khalid Muharam kutoka Lebanon alisema kua: “Katika kuhitimisha kongamano la kimataifa la Ameed awamu ya nne, tunatoa shukrani kubwa kwa watafiti wote mlio shiriki na wageni wetu watukufu, pia tunawapa pole kutokana na uchovu wa safari mliovumilia hususau ndugu zetu wairaq mliotoka mbali, tunamuomba Mwenyezi Mungu adumishe kongamano hili, tuendelee kukutana kila mwaka kwa ajili ya kuitumikia elimu na kuuenzi ujumbe mtukufu wa kiislamu”.

Akaongeza kusema kua: “Kongamano lilifungwa baada ya kutolewa wasia na maoni mbalimbali kutoka kwa washiriki, tunakuleteeni baadhi za wasia na maoni muhimu kama ifuatavyo:

  • 1- Ili kuzifanyia kazi mada za Amani na utamaduni, kongamano linaomba serikali ianzishe kamati maalumu katika kila mji, itakayo husisha mahatibu (wazungumzaji) watakao ratibu na kuhakikisha zinatolewa mada za kulingania amani.
  • 2- Kongamano limependekeza kuanzishwa kamati maalumu ya wataalamu waki-iraq, itakayo simamia utekelezaji wa sheria zilizopo.
  • 3- Kongamano limehimiza umuhimu wa kuifanyia kazi sheria ya lugha salama namba 14 ya mwaka 1977, ili kuhakikisha usalama wa lugha ambao ni msingi muhimu katika swala zima la amani na utamaduni.
  • 4- Kufungua taasisi maalumu itakayo kua mlezi wa vyombo vya habari, itakayo visimamia na kuvielekeza mambo muhimu yatakayo saidia kujenga jamii yenye maadili mema.
  • 5- Kongomano limebaini umuhimu mkubwa wa amani na utamaduni na limependekeza swala hili liingizwe katika selibasi za masomo, hivyo inawaomba wahusika kuangalia swala hili kwa umakini, kwani ni msingi muhimu katika kutengeneza jamii bora, na wamependekeza kongamano la Ameed lijalo la awamu ya tano liwe na anuani isemayo (Selibasi za masomo zilenge: uzalendo, ufafanuzi na maandalizi).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: