Kituo cha Alkafeel na studio ya Aljuud ya Atabatu Abbasiyya tukufu zimeshiriki katika kongamano la kumi na moja la kimataifa Al-Ghadiir linalo fanyika katika mkoa mtukufu wa Najafu chini ya usimamizi wa luninga ya Al-Ghadiir, lenye kauli mbiu isemayo (Vyombo vya habari na ujumbe wa muqawama na ushindi).
Ushiriki ulikua katika sekta ya vyombo vya habari vya Atabatu Abbasiyya tukufu (Luninga, redio na magazeti), pia walionyesha kazi zilizofanywa na kituo cha habari pamoja na studio, ambazo zilitengenezwa na watumishi wa Ataba tukufu ambao ni raia wa Iraq, hivyo tunaweza kusema ni zao halisi la wananchi wa Iraq.
Studio ya Aljuud ilionyesha vipande vya picha walizo tengeneza vya filamu za (Sayyidul-maau) inayo elezea nafasi ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika vita ya Twafu, vilevile walionyesha picha ya (Harhuur Almushaakis) ambayo ni mtiririko wa filamu za malezi na maadili mema kwa vijana.
Huku kituo cha uzalishaji cha Alkafeel kikishiriki kwa kuonyesha baadhi za filamu walizo tengeneza, kama vile falamu ya (Mkubwa wa maswahaba) ambayo inamuelezea Abutwalib (a.s) na filamu ya (Bibi wa makuraishi) ambayo inaelezea hatua muhimu alizopitia mama wa waumini bibi Khadija (a.s).
Kiongozi mkuu wa luninga (tv) ya Alghadiir na katibu mkuu wa kongamano hili Ustadh Mudhar Bukaau, alikaribisha ushiriki huo na akasifu ushiriki wa Atabatu Abaasiyya katika kongamano hili ambalo hua na maendeleo makubwa kila linapo fanyika, na hushuhudia ongezeko la washiriki jambo ambalo husaidia kubadilishana uzowefu na watu wengine.
Akasisitiza kua: “Hakika kongamano hili, limepata mwitikio mkubwa sana wa vyombo vya habari na vituo vya uzalishaji pamoja na vituo vya mitandao ya kielektronok na mawakala wa habari wa kitaifa na kimataifa katika ulimwengu wa kiislamu kutoka katika nchi (20), kongamano lilihushisha vipindi vya nadwa na mashindano, kulikua na zawadi (36) kila chombo cha habari kilikua na haki ya kushiriki katika mashindano hayo, yanayo husu kuelezea nafasi ya habari katika kupambana na misimamo mikali, utukufu wa habari, mwanamke na familia katika uislamu, habari za baada ya vita pamoja na nadwa zilizokua na maudhui mbalimbali”.