Zimebaki saa chahe kutangazwa kwa msimu wa huzuni na maombolezo..

Maoni katika picha
Zimebaki saa chahe kubadilishwa kwa bendara tukufu za kubba mbili, ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kushushwa bendera nyekundu na kupandishwa bendera nyeusi, ikiwa kama ishara ya kuingia mwezi wa huzuni, mwezi mtukufu wa Muharam, Mwezi ambao aliuawa mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) na watu wa nyumbani kwake (a.s), tukio hili ni miongoni mwa maandalizi maalumu ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imeandaliwa sehemu maalumu litakapo endeshwa zoezi hilo, ambapo ni uwanja wa mbele ya mlango wa Kibla katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), sehemu hiyo imesha wekewa mambo yete yanayo hitajika.

Shughuli ya kubadilisha bendera itakua na ratiba ndongo, miongoni mwa ratiba hiyo, kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya ataongea, kisha ataongea rais wa wakfu ya shia, halafu moja ya mikoa ya Iraq utapewa pendera ya maombolezo, baada ya hapo itaanza shughuli ya kushusha bendera nyekundu na kupandishwa bendera nyeusi katika kubba tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), shughuli hiyo itakamilishwa kwa qaswida za maombolezo.

Kumbuka kua jambo hili pamoja na vikao vya maombolezo limekua likifanyika tangu mwaka 2004 miladiyya, katika shughuli hiyo ndipo hutangazwa rasmi kuingia mwezi wa huzuni, na hufanyika katika mji wa Karbala makao makuu ya maombolezo ya Imamu Husseia (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: