Kitengo cha minasabati na vikundi vya Husseiniyya chatoa maelekezo kuhusu maombolezo ya Ashura na chasisitiza umuhimu wa kuzingatiwa kwa maelekezo hayo..

Maoni katika picha
Kitengo cha minasabati na vikundi ya Husseiniyya vya Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu chini ya Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) chatoa maelekezo kuhusu maombolezo ya Ashura na utaratibu wa kutoa huduma, na kimesisitiza umuhimu wa kuzingatiwa kwa maombolezo hayo, maelekezo yenyewe ni haya yafuatayo:

 • 1- Watu wote wanaotoa huduma wanatakiwa kuswali mara tu wasikiapo adhana katika maeneo yao.
 • 2- Viongozi wote wa mawaakib (vikundi) vya Husseiniyya wanatakiwa kufuata maelekezo yetu kuhusu nyakati za kufanya matembezi ya maombolezo hususan (wapiga Zanjil) kwa ajili ya kuzuia muingiliano na msongamano katika matembezi.
 • 3- Kuzingatia maelekezo yote yatakayo tolewa na watu wa usalama, kwa ajili ya kutotoa nafasi kwa maadui wa uislamu na madhehebu ya Ahlulbait (a.s).
 • 4- Kuzuia kuingia watu wasio julikana katika misafara ya matembezi ya maombolezo na kuhakikisha watu hawabebi siraha.
 • 5- Idara ya Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) hawata wajibika zaidi ya kupanga muda na kutoa maelekezo kwa viongozi wa mawaakib (vikundi), ambapo watatakiwa kuonyesha nembo (alama) maalumu za vikundi vyao na kufuata kanuni na taratibu wakati wa matembezi yao hususan watakapo ingia katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu.
 • 6- Kiongozi wa maukib (kikundi) atawajibika kuangalia usalama wa kikundi chake na kusimamia vipaza sauti.
 • 7- Kila maukib (kikundi) kitaruhusiwa kuingia na kamera moja tu, na ishikwe na mtu atakaye kua amevaa kitambulisho (baji).
 • 8- Tunatarajia wasomaji wa qaswida za maombolezo waheshimu muda walio pewa ambao ni dakika kumi tu, kutokana na wingi wa mawaakib (vikundi), na kuepuka msongamano unao weza kusababisha kusimama kwa matembezi ya maombolezo.
 • 9- Mawaakibu (vikundi) vyote vya zanjil vinatakiwa kuzingatia muda wa kuingia walio pangiwa, ambao ni kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa tisa baada ya Adhuhuri, kwani mawaakib (vikundi) vya matam vitaanza kuingia saa tisa baada ya Adhuhuri hadi katikati ya usiku.
 • 10- Hairuhusiwi kuingia Farasi watakao shiriki katika matembezi ya maombolezi katika Ataba mbili tukufu kwa ajili ya kulinda usafi na heshima ya maeneo haya matakatifu.
 • 11- Baada ya adhana ya Adhuhuri katika siku ya kumi ya Muharam kutakua na muhadhara wa maombolezo.
 • 12- Baada ya siku ya 13 Muharam inatakiwa vifaa vyote viwe vimeondolewa.
 • 13- Likitokea tangazo lolote la hatari (Allah atuepushie) watu wote wanatakiwa kuondoka katika barabara kuu haraka, kuwapisha walinda usalama (askari) kufanya jukumu lao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: