Ubaidullahi bun Ziyadi alizuia wairaq kumnusuru Imam Hussein, (a.s) wajukuu wao wamjibu kwa kuwashinda wafuasi wake madaesh, na wahuisha ahadi yao kwa Imam katika maombolezo ya Ashura..

Maoni katika picha
Mwezi nne Muharam mwaka wa (61) hijiriyya, Ubaidullahi bun ziyadi alisimama katika mji wa Kufa na akakemea vikali mtu yeyote atakaye msaidia Imam Hussein (a.s), na akasema kua atakaye toa msaada wowote kwa Imam Hussein (a.s) atauawa, na akampa Qadhi Sharihi asome waraka ulio halalisha kuuawa kwa Imam Huseein (a.s), na akaamuru kufungwa njia zote zinazo ingia katika mji wa Kufa, ili kuzuia watu wa Kufa na kutoka katika miji mingine wasiende kumnusuru Imam (a.s).

Leo baada ya miaka (1400) bado wafuasi wa Imam Hussein na wapenzi wake wanapambana na kila anaye jaribu kuzima harakati ya Imam Hussein, katika vita ya kuwang’oa magaidi ya Daesh wameonyesha ujasiri na ushujaa wa hali ya juu kabisa, na wamezima njama zote za maadui wa Iraq.

Huenda siri kubwa katika hili ni malezi waliyo pata majemedari hawa, yaliyo jaa mafundisho ya Imam Hussein (a.s) yenye msingi wa kauli yake isemayo “Sitakupeni mkono wangu kiudhalili”, ni wazi kua siri ya ujasiri wao mbele ya wauwaji wa Imam Hussein (a.s) inatokana na imani yao kuhusu uhalali wa harakati hiyo, sasa wanasema kwa kinywa kipana kua: Mlituzuia kumnusuru Imam Hussein na watu wa nyumani kwake (a.s) kabla ya miaka (1400), hakika nyie wajukuu wa Ubaidullahi bun Ziyad hamuwezi na hamtaweza kuondoa mapenzi yetu na kutuzuia kuilinda sehemu hii takatifu.

Jibu lingine lililotolewa na watu wa Imam Hussein (a.s) katika mji wa kujitolea muhanga, mji wa mashahidi wa Karbala, ni jibu la kuonyesha kushindwa kwa jeshi ya Umawiyya lililofanya kila aina ya ukatili na vitisho katika mwaka wa 61 hijiriyya, kwa ajili ya kuzima harakati ya Imam Hussein (a.s), lakini matashi ya Mwenyezi Mungu hayakua kama wanavyo taka wao, leo hii vikundi vya kuomboleza kifo cha Imam (a.s) vimevunja vikwazo vyote vilivyo wekwa na ibun Ziyadi wakati ule kupitia kwa Qadhi Sharihi aliye halalisha kuuawa kwa Imam Hussein (a.s), wanainua sauti zao na kusema “Yaa Hussein.. Yaa Hussein” wanahuisha harakati ya Imam Hussein na kufuata mwenendo wake, na kuonyesha utayari wao wa kumnusuru Imam pamoja na kupita kwa muda mrefu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: