Msimamo wa Abulfadhil Abbasi (a.s) usiku wa mwezi kumi Muharam..

Maoni katika picha
Wanahistoria wanasema kua; Imamu Hussein (a.s) aliwakusanya maswahaba wake na watu wa nyumani kwake katika usiku wa Muharam kumi, akawaambia kua; Hakika watu hawa (maadui) hawamtaki mtu mwingine yeyote zaidi yake, na akawaruhusu waondoke: “Fahamuni kua siku yetu na maadui hawa ni kesho, mimi nimewaruhusu nyie wote muondoke, wala hamna lawama kwangu, usiku huu utumieni kwa safari, kila mtu ashike mkono wa ngugu yake na muondoke, Mwenyezi Mungu atakulipeni kheri, tumieni giza hili kila mmoja arudi nyumbani kwake”.

Mtu wa kwanza aliye simama na kumjibu alikua ni ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), alizungumza maneno ya mlinzi muaminifu na makini, jawabu lililofungua njia kwa wengine nao wakajua cha kumjibu Imamu wao Hussein (a.s), walionyesha msimamo wa uaminifu na ushujaa, wakapata utukufu wa duniani na akhera.

Hakika alisimama na akasema: “Kwanini tufanye hivyo (tuondoke)! Ili tubaki hai baada yako? Hapana Mwenyezi Mungu asituonyeshe siku hiyo”.

Na wengine wakasimama na kusema maneno yanayo fanana na maneno haya, Imamu Hussein (a.s) akawashukuru kwa msimamo mzuri walio onyesha, akasifu imani yao na ikhlasi ya hali ya juu waliyo nayo: “Mimi sifaham maswahaba wazuri na waaminifu kama maswahaba wangu, wala ngugu wema na wenye upendo kama ndugu zangu, Mwenyezi Mungu akulipeni kila la kheri kwa ajili yangu”.

Abulfadhil Abbasi (a.s) alikua mtu wa kwanza kuonyesha msimamo huo na kupata utukufu mkubwa kutokana na uaminifu wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: