Jumla ya maukibu (vikundi) vya kitaifa na kigeni zaidi ya (1500) wameshiriki katika ziara ya Ashura..

Maoni katika picha
Rais wa kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya hapa Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu, chini ya Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) Haji Riyadh Niimah Salmaan, amesema kua idadi ya maukibu na vikundi vya Husseiniyya vilivyo shiriki katika maombolezo ya Ashura mwaka huu ni zaidi ya (1500) tukijumuisha vya nchini na vya kigeni mwaka huu wa 1439 hijiriyya.

Akaongeza kusema kua: “Mawakibu (vikundi) vilikua vya aina mbili, aina ya kwanza ni vikundi vya Matam na Zanjiil na aina ya pili ni vikundi vya watoa huduma, pia vipo baadhi ya vikundi vilikusanya mambo yote mawili (Matam na Zanjiil pamoja na kutoa huduma) na vyote hivyo ni vya wakazi wa Karbala, siku kumi za kwanza katika mwezi wa Muharam ni rasmi kwa ajili ya watu wa Karbala tu, hali kadhalika kulikua na ushiriki wa vikundi kutoka Baharain, Lebanon, Kuwait, Iran, India na Pakistan”.

Akabainisha kua: “Idadi hii ni zile maukibu (vikundi) vilivyo sajiliwa kwetu na katika idara za usalama za mpakani mwa mkoa mtukufu wa Karbala, pia kuna vikundi vingi vinatoa huduma kwa mazuwaru bila kusajiliwa kwetu wala katika idara za usalama za mipakani, ikiwa ni pamoja na makumi ya nyumba zinazo fungua milango yao na kutoa huduma kwa watu wanaokuja kufanya ziara kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kumbuka kua kitengo cha mawakibu kilifanya usajili rasmi wa mawakibu na vikundi vya Husseiniyya na kuwapa vitambulisho maalumu, pia kilifanya vikao mara kadhaa vya maandalizi pamoja na viongozi wa vikundi hivyo kabla ya kuanza kwa msimu wa ziara ya Ashura, kwa ajili ya kuhakikisha wanatoa huduma bora zaidi na kuondoa aina zote za vikwazo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: