Kwa mara ya kwanza katika Aridhi ya Karbala tukufu kikundi cha Zaharaa (a.s) chaonyesha igizo la Twafu.

Maoni katika picha
Historia imebainisha utukufu wa kudumu na umuhimu wa kutumia maigizo, toka karne za mwanzo watu waliigiza tukio la Imamu Hussein (a.s), ili kubakiza ujumbe halisi wa harakati yake ya Muhammadiyya, uliobeba fikra za uislamu sahihi aliokua akiuwakilisha yeye, na kufichua njama za watu wanaotaka kuupotosha na kuharibu misingi mitukufu ya uislamu, maigizo hayo yanaangazia vipengele vya tukio zito ambalo Imamu Hussein (a.s) anasema: “Hakuna siku nzito kama siku yako ewe Abuu Abdillah”.

Jambo hili limetufanya tutamani kuja katika aridhi halisi ya Karbala, tukiwa na kundi la vijana kutoka katika mkoa wa Diwaniyya mtaa wa Ghamaas, tukiwa na matarajio ya kufikisha ujumbe wao kupitia igizo la vita ya Twafu, baada ya kumtegemea Mwenyezi Mungu, tumefanyia kazi riwaya zilizo hakikiwa na wanachuoni wakubwa wa Najafu.

Kwa mara ya kwanza igizo hili linafanyika katika aridhi ya Karbala, tulikua tunalifanyia katika aridhi ya Ghumaas kwa kipindi cha miaka tisa, igizo hili hurejesha fikra za watu katika matatizo aliyo pata Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) siku ya mwezi kumi Muharam.

Haji Haadi Atwishaan Shimraan kiongozi wa kikundi za Zaharaa (a.s) amesema kua: “Kikundi cha Zaharaa (a.s) kinafanya igizo la vita ya Twafu katika aridhi ya Karbala kwa mara ya kwanza, igizo linalo onyesha namna Imamu Hussein (a,s) alivyo dhulumiwa pamoja na watu wa nyumbani kwake (a.s) na maswahaba zake watukufu, mambo waliyo fanyiwa katika siku ya mwezi kumi Muharam mwaka wa (61) hijiyya, maandalizi ya igizo hili yamefanyika kwa zaidi ya miezi sita, baada ya kupata kibali cha balaza la mkoa wa Karbala na kitengo cha mawakibu (vikundi) vya Husseiniyya cha Ataba mbili (Husseiniyya na Abbasiyya) tukufu, tulianza kuandaa mahema na kufanya mazoezi tukiwa katika mji wa Ghamaas, tukaona kua; mwaka huu ni vyema maonyesho ya igizo hili yafanyike katika aridhi ya Karbala, aridhi takatifu, aridhi ya shahada na utukufu”.

Akaongeza kusema kua: “Idadi ya watu wanao igiza upande wa jeshi ya Umawiyya ni (1200), na watu wanao igiza upande wa maswahaba wa Imamu Hussein ni kati ya (30 hadi 35), pamoja na kundi la wanawake na watoto, riwaya tulizo tumia katika kuandaa igizo hili tulizifanyia uhakiki kupitia kwa wanachuoni wakubwa wa mji mtukufu wa Najafu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: