Matembezi ya maombolezo: Scaut ya Alkafeel wahuisha ahadi yao kwa Imamu Hussein na ndugu yao Abulfadhil Abbasi (a.s).

Maoni katika picha
Scaut ya Alkafeel chini ya idara ya watoto na makuzi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kama kawaida yake kila mwaka, wamemuahidi Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kufuata mwenendo wao na kuwafanya taa linalo angazia maisha yao, vilevile wamehuisha maombolezo na kutuma rambirambi kwa Swahibu Zamaan (a.f) kufutia kumbukumbu ya kuuawa kwa babu yake Abuu Abdillahi Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) pamoja na maswahaba wake watukufu.

Katika matembezi ya maombolezo yaliyo fanyika jioni ya siku ya Juma Mosi (16 Muharam 1439h) sawa na (07/10/2017m) chini ya anuani isemayo: (Iraq ya Hussein itabakia kua moja).

Katika matembezi haya wameshiriki zaidi ya wanascauti 200, wakiwa wamebeba mabango ya maombolezo, matembezi yalianzia katika eneo la mlango wa Bagdad (Baabu Bagdad) na kuelekea katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) huku wakiimba qaswida za huzuni na maombolezo, wakaishia katika haram ya Abuu Abdillahi Hussein (a.s) kwa kufanya majlisi ya maombolezo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: