Kwa picha: Hivi ndivyo walivyo adhimisha watumishi wa Abulfadhil Abbasi siku ya saba ya kuuawa kwa Imamu Hussein (a.s)..

Maoni katika picha
Wafuasi wa Ahlulbait (a.s) wamezoea kuadhimisha siku ya saba toka kuuliwa kishahidi kwa Imamu Hussein (a.s), kwa kuonyesha huzuni na kufanya maombolezo, hakika kuuawa kwa Imamu Hussein (a.s) kutaendelea kua na majonzi makubwa kwa waumini hadi atakapo dhihiri Imamu Hujjah bun Hassan (a.f).

Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) katika mwezi kumi na saba Muharam (siku ya saba tangu kuuawa kwa Imamu Hussein –a.s-), wamehuisha huzuni na kutoa pole kwa Imamu wa Zama (a.f), kutokana na msiba huu mkubwa, huku mazingira yao yakisema:- Ikiwa hakuhudhuria yeyote siku ya saba ya kuuawa kwako ewe kiongozi wetu, sisi watumishi wako leo tunakuja katika kaburi lako na kufanya maombolezo.

Msafara ulianzia ndani ya malalo ya mmbeba bendera ya Imamu Hussein (a.s) Mwezi wa Baniy Hashim Abulfadhil Abbasi (a.s), wakaelekea katika malalo ya Bwana wa mashahidi (a.s) kufanya taazia kutokana na msiba huu mkubwa, wakiwa wamebeba mishumaa kama ishara kua siku ya saba hakukua na yeyote wa kuwasha mshumaa katika kaburi la Imamu Hussein (a.s).

Matembezi yao yalipambwa na kaswida pamoja na maneno ya kuomboleza watu wa nyumba ya Mtume (a.s), ambayo yalionyesha mapenzi ya watumishi wa Ataba mbili tukufu kwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s), na kushikamana kwao na mwenendo wa Imamu Hussein (a.s) pamoja na kuenzi damu yake takatifu iliyo endeleza dini ya babu yake Mtume mtukufu (s.a.w.w), na wakafanya majlis ya maombolezo katika haram yake tukufu.

Hakika tukio la mauaji ya Twafu linaumiza sana roho za waumini, daima litaendelea kukumbukwa na kuombolezwa na wapenzi wa Abuu Abdillahi Hussein (a.s), kila mtu hujiandaa kufanya maombolezo haya kinafsi, kimwili na kiakili, hakika mafungamano haya hua na matokeo mazuri katika mazingira halisi ya maisha.

Huanza kumbukumbu ya maombolezo haya kufuatia kuwasili kwa Imamu Hussein (a.s) katika aridhi ya Karbala siku ya mwezi pili Muharam, pamoja na yaliyo jiri katika siku hizo, na huendelea hadi Muharam kumi, siku yenye majonzi zaidi, huanza usiki wa mwezi kumi hadi jioni yake, na huendelea hadi mwezi kumi na tatu, ambayo ni siku ya tatu tangu kuuawa kishahidi kwa Imamu Hussein (a.s), kisha hufuatia siku ya mwezi kumi na saba, ambayo huitwa siku ya saba toka kuuawa kwa Imamu, hivi ndivyo ambavyo hufanywa maombolezo ya msiba huu mkubwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: