Watu wa Karbala wamewasha mishumaa na kububujika majozi, wakihuisha siku ya saba tangu kuuawa kwa Imamu Hussein (a.s)..

Maoni katika picha
Kama hawakuhudhuria watu wa nyumbani kwako na wapenzi wako katika kaburi lako ewe Abu Abdillahi Hussein katika siku ya saba ya kuuawa kwako mwaka (61h), na wala hakuna aliye kuwashia mishumaa na kumwagia kaburi lako maji pamoja na kufanya maombolezo, hawa hapa wapenzi wako na wafuasi wako watu wa Karbala wamekuja kuomboleza na kumpa pole mama yako Zaharaa (a.s) na babu yako Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), kutokana na msiba huu mkubwa ambao haujapoa na katu hautapoa zama na zama.

Watu wa Karbala kupitia vikundi vyao mbalimbali wamefanya maombolezo hayo kama kawaida yao kila mwaka, ifikapo siku ya saba tangu kuuawa kwa Imamu Hussein (a.s), baada ya swala ya Magharibi na Ishaa hujitokeza kwa pamoja watu wa Karbala na kufanya maombolezo na kumpa pole bibi Zainabu (a.s) kutokana na misukosuko mikubwa iliyo msibu mfululizo.

Yamekua ni mazoea ya watu wa Karbala kwa muda mrefu, walielekea katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) baada ya kutoka katika haram ya Abu Abdillahi Hussein (a.s), wakiwa wanaimba kaswida za maombolezo huku wamebeba mishumaa, kama sehemu ya kumkumbuka na kumuenzi bibi Zainabu (a.s), walipo ingia katika haram wakafanya majlisi ya maombolezo iliyo hutubiwa na Shekh Bahaau Karbalai mtoto wa marehem Shekh Haadi Karbalai, baada yake akaingia mwimbaji wa kaswida Abdul-Amiri Umawiy, wahadhiri na waimbaji wote walikumbusha yaliyo jiri kwa Imamu Hussein (a.s) na mateka watukufu.

Fahamu kua tukio la mauaji ya Twafu huombolezwa na kila mtu, uhuishaji wa kumbukumbu ya maombolezo haya hupewa umuhimu na wapenzi wote wa Abu Abdillahi Hussein (a.s), hivyo kila mtu hujiandaa kufanya maombolezo haya kiroho, kimwili na kiakili, maandalizi hayo humfanya kila mtu kutumia fursa na kuonyesha hisia zake na kushikamana kwake na Imamu katika utendaji wa maisha yake ya kila siku.

Huanza maombolezo rasmi kufuatia kuingia kwa Imamu Hussein (a.s) katika Aridhi ya Karbala mwezi pili Muharam, na huendelea kukumbukwa mambo yote yaliyo jiri katika siku hizo, na huendelea hadi mwezi kumi Muharam ambayo ndio siku yenye huzuni zaidi, kisha siku ya mwezi kumi na tatu (yaani siku ya tatu tangu kuuawa kwa Imamu Hussein a.s), kisha hufuatia siku ya mwezi kumi na saba Muharam, siku ya saba toka Kuuawa kwake, ndio maana unaona vikundi vya waombolezaji wakifanya maombolezo ya msiba huu mkubwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: