Kamati ya misaada chini ya ofisi ya Marjaa dini mkuu, waendelea kutoa misaada katika miji iliyo kombolewa hivi karibuni, na wakazi wa miji hiyo watoa shukrani zao..

Maoni katika picha
Wakazi wa miji iliyo kombolewa hivi karibuni na jeshi la serikali kwa kushirikiana na Hashdi Sha’abi, kutoka mikononi mwa magaidi wa Daesh, ambayo ni miji ya; Sharqaat, tarafa ya Zaab na wilaya ya Huweijah, wametoa shukrani nyingi kwa Marjaa dini mkuu, kutokana na misaada yake ya kibinadamu na namna alivyo karibu nao katika mazingira magumu wanayo pitia, kamati ya misaada ilienda kuwatembelea na kuangalia hali yao, jambo hili linaonyesha wazi namna Marjaa dini mkuu alivyo kua na huruma ya mzazi kwa wanaye, hakika kama sio fatwa yake tukufu miji hii isinge kombolewa kutoka mikononi mwa magaidi wa Daesh hadi sasa.

Hayo yamesemwa kufuatia shehena ya hivi karibuni ya misaada katika miji iliyo kombilewa ya Isdira ya juu, ya kati na ya chini pamoja na kijiji cha Twaqtwaq, I’lila, Swahani na tarafa ya Zaab pamoja na vijiji vya Shamiit, Namiswa na kijiji cha Aklah kilichopo katika Tarafa ya Zaab, msafara huo wa misaada umegawa jumla ya vikapu (3500) vilivyo jaa aina mbalimbali za vyakula, pamoja na maziwa ya watoto na vitu vingine.

Kumbuka kua shehena hii ya misaada ni sehemu ya mpango kabambe wa Marjaa dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani wa kusaidia wakimbizi katika miji yote iliyo kumbwa na vita, pia hutoa huduma mbalimbali kwa wakimbizi hao, kamati hii iliundwa siku za mwanzo kabisa na ikaanza kutoa misaada kwa familia za wakimbizi na kila mtu aliye athiriwa na magaidi wa Daesh.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: