Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu akutana na watalamu wa idara ya uzalishaji ya Alkafeel, na asifia kazi nzuri waliyo fanya katika kipindi cha ziara ya Ashura..

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmad Swafi, amesifu kazi nzuri iliyo fanywa na watalamu wa idara ya uzalishaji ya Alkafeel, chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, hususan upande wa picha za video, ambazo huonyesha picha halisi za matukio kupitia matangazo ya moja kwa moja yaliyo onyesha mawakibu na vikundi vya maombolezo na shughuli zao.

Ameyasema hayo alipo kutana na watalamu wa idara hiyo kitengo cha picha za mnato na video.

Aidha amewataka kuongeza juhudi na kuboresha zaidi kazi zao, pia wasilizike na kiwango fulani, bali kila siku wafikilie kujiendeleza zaidi ili waendane na utukufu wa mtu wanaye mtumikia mwenye malalo haya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Mwisho Sayyid Swafi aliwaombea mafanikio mema katika kazi zao watumishi wa idara hii na akamuomba Mwenyezi Mungu azijaalie katika mizani ya mema yao.

Kumbuka kua idara ya uzalishaji ya Alkafeel kupitia matangazo ya moja kwa moja, iliweza kurusha matukio ya maombolezo ya Ashura kuanzia siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Muharam (tukio la kubadilisha bendera) na bado wanaendelea hadi mwezi ishirini Safar, vyombo vingi vya habari vya kitaifa na kimataifa vimenufaika kutokana na huduma ya matangazo ya moja kwa moja, kwani yanarushwa bila kutumia program ya ndani (local).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: