Katika siku ya tatu ya kongamano la msimu wa Ashura linalo endelea katika mji wa Takab huko Iran, chini ya usimamizi wa Atabatu Husseiniyya tukufu na ushiriki wa Atabatu Kadhimiyya na Abbasiyya, limeshuhudia mambo mengi, miongoni mwa ratiba zake ni muhadhara elekezi ulio tolewa na Sayyid Imaad Hakiim ambaye ni Ustadh katika Hauza ya Qum, alizungumzia mambo yanayo husiana na namna ya kutengeneza familia, akasema kua jambo hilo ni muhimu sana kwani ndilo hujenga jamii.
Sayyid Imaad Hakiim alibainisha kua: “Hakika familia ndio mbegu ya jamii yenye mafanikio, itakapo kua familia hiyo inafuata mwenendo wa Ahlulbait (a.s), ndipo tutakapo pata jamii iliyo kamilika, tukiangalia mafundisho ya kiislamu hata kwa kutumia akili tu, tutayakuta yanaukamilifu mkubwa, jamii yeyote ambayo haitafuata mafundisho ya dini tukufu ya kiislamu yaliyo fundishwa na kusisitizwa na Mtume wetu Mtukufu (s.a.w.w) itakua na mapungufu mengi.
Akasisitiza kua: “Hakika vita ya kitamaduni inayo shambulia jamii yetu ya kiislamu, inatakiwa na sisi tusimame imara kupambana nayo, wala tusiiachie ikaharibu jamii yetu, na miongoni mwa namna za kupambana na vita hii ni kwa kufanya vikao na makongamano kama haya yanayo adhimisha mambo ya kidini, na kutolewa kwa mihadhara inayo fafanua mambo yenye utata miongoni mwa mafundisho ya dini yetu, nawahimiza vijana wetu wahudhurie kwa wingi katika vikao kama hivi, hususan wanaofanya kazi katika vyombo vya habari ili watusaidie kusambaza ujumbe huu kwa walimwengu”.
Katika ratiba ya leo kulikua na usomaji wa mashairi ya Husseiniyya, baada ya Qur’an tukufu iliyo somwa na Muhammad Amiri Tamimi, ambaye ni msomaji wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ikafuata zamu ya mashairi yaliyo somwa na wageni waalikwa na kuburudisha masikio ya wahudhuriaji, baada ya mashairi ikasomwa majlisi ya maombolezo ya kifo cha Imamu Zainul-Abidina (a.s), iliyo somwa na Sajaad Ahmad kutoka katika Atabatu Kadhimiyya tukufu kisha akasoma Muhammad Tamimi kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu halafu majlisi ikahitimishwa kwa kisomo cha Hamid Dhaighamiy kutoka mji mtukufu wa Qum.