Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu watembelea vikosi vya wapiganaji na kuangalia shida zao..

Maoni katika picha
Kwa ajili ya kutekeleza maagizo ya Marjaa dini mkuu, yanayo himiza kusaidia wanajeshi waliopo katika uwanja wa vita kwa ajili ya kulinda taifa, siku ya Juma Tano iliyo pita sawa na (20 Muharam 1439h) sawa na (11 Oktoba 2017m), jopo la watu kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu walienda kutembelea vikosi vya wanajeshi na Hashdi Sha’abi na kuwapa misaada mbalimbali, kama vile chakula na vitu vingine. Ujumbe huo ulihusisha mashekh na watumishi wengine kutoka katika Atabatu Abbasiyya tukufu na uliongozwa na Shekh Haidari Aaridhi kutoka katika kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu, walitembelea vikosi vilivyopo katika miji iliyo kombolewa hivi karibuni ya Huweijah na Riraadh, hali kadhalika walitembelea vikosi vilivyopo katika mpaka wa Iraq na Sirya, pamoja na jeshi la wanamaji lililopo katika mji wa Tharthar, vilevile waliwatembelea mashahidi wa Speikar na kufanya majlis ya maombolezo halafu wakagawa chakula na wakaelekeza thawabu kwa Imamu Hussein (a.s). walitembelea pia vituo vya afya vya wanajeshi wa serikali na Hashdi Sha’abi na kuwapa misaada ya dawa na vifaa tiba.

Kiongozi mkuu wa msafara Shekh Haidari Aaridhi alisema kua: “Atabatu Abbasiyy tukufu imekua ikitembelea vikosi vya wapiganaji watukufu waliopo katika uwanja wa vita na kutoa misaada mbalimbali toka kutolewa kwa fatwa tukufu na Marjaa dini mkuu hadi leo, tumefanya ziara hii kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kiseria katika Atabau Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmad Swafi, kwa ajili ya kutoa msaada wa kimaanawiyya na kimkakati”.

Kumbuka kua ziara hii imedumu siku tano, ugeni huu; umetembelea miji iliyo kombolewa siku chache zilizo pita pamoja na wanajeshi wanaolinda mpaka wa Iraq na Sirya, kila sehemu waliyo tembelea wamefanya majlis na kugawa chakula.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: