Pembezoni mwa kongamano la msimu wa Ashura siku ya nne, muhadhara ulio tolewa na maonyesho ya picha yathibitisha ushujaa wa Hashi Sha’abi watukufu..

Maoni katika picha
Miongoni mwa ratiba ya siku ya nne katika kongamano la msimu wa Ashura, wageni kutoka katika Ataba tukufu walitembelea hospitali ya mashahidi katika mji wa Takab na wakagawa zawadi za tabaruku kwa wagonjwa walio lazwa katika hospitali hiyo, ikiwa ni pamoja na kutabaruku kwa bendera ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kisha ulitolewa muhadhara kuhusu (Sha’aairi Husseiniyya) ambapo Shekh Haidari Najafiy alielezea uwelewa kuhusu Sha’aairi Husseiniyya na akataja ushuhuda wa riwaya za Ahlulbait (a.s) zinazo himiza kufanywa kwa Sha’aairi hizo, akabainisha kua: “Tunatakiwa kutambua kua, hizi sha’aairi hazipo tu bure, bali zipo kwa ajili ya kutafuta shifaa ya Imamu Hussein (a.s) na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu mtukufu”.

Miongoni mwa shughuli za leo, kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimefanya maonyesho ya picha zilizo thibitisha ujasiri na ushujaa wa Hashdi Sha’abi, walipo simama kuitikia wito wa Marjaa dini mkuu ulio tolewa katika mji mtukufu wa Najafu, picha hizo zilionyesha ubinadamu walio fanya wapiganaji hao watukufu katika kulinda uhai wa raia na mali zao, pamoja na ujasiri walio kua nao katika mapambano ya kihistoria kwa ajili ya kukomboa na kuilinda aridhi ya Iraq na maeneo matakatifu.

Fahamu kua kongamano la msimu wa Ashura linafanywa chini ya usimamizi wa Atabatu Husseiniyya tukufu katika mji wa Takab nchini Iran na kwa ushiriki wa Atabatu Kadhimiyya na Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: