Matawi ya Atabatu Abbasiyya tukufu yanaendelea na maandalizi ya kushiriki katika maonyesho ya kimataifa yatakayo fanyika Bagdad na wasisitiza kua ushiriki wao utafana..

Maoni katika picha
Kutokana na kukaribia kuanza kwa maonyesho ya kimataifa ya 44 katika mji wa Bagdad, matawi ya Atabatu Abbasiyya tukufu yatakayo shiriki katika maonyesho hayo, yatakayo anza Juma Mosi (21-30 Oktoba 2017m) chini ya kauli mbiu isemayo (Tumekomboa aridhi yetu na kwa kusaidiana kwetu tutaijenga) yanaendelea na maandalizi.

Atabatu Abbasiyya itawakilishwa na matawi yake matano ambayo ni:

  • 1- Shirika la Nurul-Kafeel linalo zalisha bidhaa za wanyama, litashiriki kwa kuonyesha bidhaa linazo zalisha.
  • 2- Shirika la Aljuud la teknolojia ya kilimo cha kisasa, litaonyesha bidhaa linazo zalisha miongoni mwa vifaa vya kusafishia, mbolea na dawa za kutibu maradhi ya mimea na wanyama.
  • 3- Shirika la Liwaau Al-aalamiyya la viwanda na biashara, litaonyesha bidhaa zinazo zalishwa na shirika hilo, ikiwa ni vifaa vya ujenzi vya aina mbalimbali.
  • 4- Darul-Kafeel ya uchapishaji na usambazaji, itaonyesha machapisho yake pamoja na baadhi ya vifaa vyao wanavyo tumia.
  • 5- Shirika kuu la uzalishaji la Alkafeel lililo chini ya kitengo cha kilimo na ufugaji, litaonyesha bidhaa za kilimo wanazo zalishwa, na mashamba ya Khairaat Abulfadhil Abbasi, pamoja na kuonyesha video za mashamba darasa na mashamba ya Anwaaru Saaqi na Qaadhi Haajaat.

Viongozi wa matawi hayo wamesisitiza kua maonyesho yao yatafana kutokana na bidhaa watakazo onyesha, pamoja na kuelezea maendeleo makubwa yaliyo fikiwa katika vitengo vyote vya Ataba tukufu katika kila sekta.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imekwisha shiriki mara nyingi katika maonyesho ya kimataifa ya Bagdad, na huyachukulia kua maonyesho muhimu kwake, pia wamesha shiriki katika maonyesho na makongamano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa, kote huonyesha bidhaa wanazo zalisha na huelezea maendeleo yanayo patikana katika Atabatu Abbasiyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: