Kutokana na uzalishaji wake wa bidhaa za viwandani, kilimo na chakula, Atabatu Abbasiyya tukufu yashiriki katika maonyesho ya kimataifa ya Bagdad..

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu yashiriki katika maonyesho ya kimataifa ya 44 mjini Bagdad yaliyo anza leo Juma Mosi asubuhi (30 Muharam 1439h) sawa na (21 Oktoba 2017m) chini ya kauli mbiu isemayo (Tumekomboa aridhi yetu na kwa kushirikiana tunaijenga), yameshiriki mashirika 400 ya kitaifa na kimataifa kutoka katika nchi 18.

Ushiriki wa maonyesho ya mwaka huu ni muendelezo wa ushiriki wa myaka ya nyuma, ambayo walipata mwitikio mkubwa na wa aina yake, mwaka huu inawakilishwa na mashirika yake matano yanayo tengeneza bidhaa za viwandani, kilimo na vyakula, ambayo ni:

(Shirika la Nurul-Kafeel linalo zalisha bidhaa za wanyama, Shirika la Aljuud la teknolojia ya kilimo cha kisasa, Shirika la Liwaau Al-Aalamiyya la viwanda na biashara, Darul-Kafeel ya uchapishaji na usambazaji pamoja na Shirika kuu la uzalishaji la Alkafeel lililo chini ya kitengo cha kilimo na ufugaji).

Mashirika hayo kila moja litaonyesha bidhaa linazo zalisha, na kauli mbiu yao inasema (Viwanda ndio fahari ya Iraq). Ushiriki wa Atabatu Abbasiyya katika maonyesho haya unachangia kuonyesha ubunifu wa wafanya kazi wake katika kuleta maendelea, na kuonyesha shughuli mbalimbali zinazo fanywa na vitengo vyake katika sekta ya viwanza, ujenzi, kilimo pamoja na uzalishaji wa chakula, pia kunatoa nafasi ya kuangalia bidhaa zinazo zalishwa na mashirika mengine yanayo shiriki katika maonyesho, hakika hii ni fursa kubwa ya kuwasiliana na mashirika ya kitaifa na kimataifa yanayo shiriki maonyesho.

Pia ushiriki huu unatuma ujumbe kwa walimwengu kua, pamoja kua Atabatu Abbasiyya tukufu ni mahala pa kufanya ibada, vilevile imekua taasisi ya kielimu, kitamaduni na kiviwanda, yoto haya inafanya kwa ajili ya kuhakikisha wanatoa huduma bora zaidi kwa watu wanaokuja kufanya ziara kwanza, kisha anafuata mwananchi wa Iraq, kinacho onyeshwa katika maonyesho haya ni kidogo sana miongoni mwa Barakaati za Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu wamesha shiriki katika maonyesho na makongamano mbalimbali ya ndani na nje ya Iraq, maonyesho ya kimataifa ya Bagdaq huyachukulia kwa umuhimu mkubwa na huanza kujiandaa mapema kwa ajili ya maonyesho hayo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: