Kuwasili Sham kwa mateka wa Ahlulbait (a.s)..

Maoni katika picha
Baada ya kamalizika vita ya Twafu na kuuawa kishahidi kwa Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake watakatifu (a.s), yalianza mateso mengine yenye kuumiza, ikiwa ni kutekwa kwa Ahlulbait (a.s) na kuwatembeza kutoka Karbala hadi Kufa, kisha kutoka Kufa hadi Sham, huku wakiwa wametanguliwa na vichwa vya wapenzi wao vikiwa vimetungikwa juu ya mikuki, hakika sehemu hii inamachungu makubwa yenye kuumiza.

Katika siku kama ya leo, mwezi mosi Safar mwaka (61h) ndio siku ambayo waliwasili mateka wa Ahlulbait (a.s) huko Sham. Majlisiy anasema katika kitabu cha Bihaar kua: kutoka kwa Sahal bun Saadi Saaidiy anasema: Nilitoka kuelekea Baitul-Muqadas, nilipo fika katikati ya Sham, nikatokea sehemu yenye mto unaotiririrsha maji na pana uoto mzuri wa miti, nikakuta watu wamefunga pazia na kuweka vizuizi huku wakisherehekea, na palikua na wasichana wanacheza ngoma, nikajiuliza! Hakuna sikukuu yeyote ya watu wa Sham ispokua naijua sasa hii ni sikukuu gani!!? Nikawaona watu wanaongea, nikawafuata na kuwauliza, nikasema: mimi ni Sahal bun Saadi nilimuona Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Wakasema: Ewe Sahal! Haikufurahishi mbingu kutonyesha damu na aridhi haimezi watu. Nikasema: kuna nini? Wakasema: Hiki hapa kichwa cha Hussein familia ya Mtume (s.a.w.w) kimeletwa kutoka Iraq. Nikasema: Ajabu iliyoje kinaletwa kichwa cha Hussein na watu wanafurahi, nakauliza: Wataingilia mlango gani? Wakanionyesha mlango unao itwa: Mlango wa saa.

Akasema: Nilipo kua hapo ghalfa nikaona bendera zinafuatana, kisha nikamuona mpanda farasi akiwa amebeba kichwa kinafanana sana na sura ya Mtume (s.a.w.w), na nyuma yake kuna wasichana nikawafuata na kumuuliza mmoja wao; Ewe dada ni nani wewe? Akajibu: Mimi ni Sukaina bint Hussein (a.s). Nikamuuliza unashida yeyote kwangu? Mimi ni Sahal bun Saadi, nilimuona babu yako na nikasikia maneno yake, akasema: Ewe Sahal, muambie huyu aliye beba kichwa atangulie mbele ili watu washughulike na kuangalia kichwa na wasituangalie sisi, Sahal anasema: Nikamfuata mbebaji wa kichwa nikamuambia: Je! Unaweza kunisaidia shida yangu? Na nitakupa dinari mia nne. Akasema: Shida gani? Tanguliza kichwa hiki mbele ya watu wa nyumba ya Mtume, akakubali na akafanya hivyo na mimi nikampa hela niliyo muahidi.

Sahal bun Saadi Saaidiy akasema: Nikamgeukia Ali bun Hussein (a.s) na kumuambia: Maulaaya unashida yeyote? Akaniambia: Je! Unahela? Nikasema: Ninayo dinari elfu moja, akasema: toa kiasi cha hela umpe aliye beba kichwa na umuambie atembee mbali na wanawake. Sahal anasema: Nikafanya hivyo na nikarudi kwake na kumuambia Maulaaya nimetekeleza ulicho niamrisha, Nikamuuliza: Je! Unashida nyingine? Akasema: Ewe Sahal je unaguo kuukuu? Nikasema: Ewe bwana wangu, utaifanya nini? Nyie hua mnagawa nguo za thamani kwa watu halafu unaniuliza nguo kuukuu? Akasema: Ewe Sahal nataka niiweke chini ya mnyororo hakika umeniumiza shingo langu, Sahal akasema: Nikampa nguo, alipo inua mroro damu zikatoka sehemu ile.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: