Kutokana na imani iliyojaa mapenzi na kwa ajili ya kupendezesha muonekano wa mazaru za Karbala tukufu, watumishi wa idara ya utunzaji wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kufuatia maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria, wameagizwa kufanya usafi na ukarabati wa malalo ya Huru bun Yazidi Riyahi (a.s).
Watumishi zaidi ya (28) wa idara tajwa hapo juu katika Ataba ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wanafanya kazi ya kukarabati maraya (marumaru za vioo) na mapambo pamoja na kila kitu kinacho husiana na ukarabati, ikiwa ni pamoja na kubadilisha taa, kazi hii imefanywa mfululizo usiku na mchana.
Haji Hassan Hilali ambaye ni kiongozi wa kitengo cha utunzaji wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ameumbia mtandao wa Alkafeel kua: “Baada ya kupokea maombi kutoka katika malalo ya Huru bun Yazidi Riyahi uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu uliona umuhimu wa kupeleka watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwenda kuyafanyia ukarabati mapambo na maraya yaliyopo katika malalo hiyo tukufu na kufaya kazi ya ukarabati na usafi kwa ujumla, ndipo idara ya mapambo na maraya ikaagizwa rasmi na kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) kupeleka wataalamu wake kwenda kufanya kazi hiyo”.
Akaongeza kusema kua: “Watumishi hao wamefanya kazi wiki mbili mfululizo kila siku, walikua na zamu mbili ya asubuhi na jioni, wamebadilisha taa zote, na kufanyia matengenezo mapambo na maraya zilizopo katika haram hiyo tukufu, pamoja na kusafisha madini ya fedha yaliyopo katika kaburi tukufu”.
Fahamu kua kitengo hiki cha utunzaji wa haram kabla ya miezi michache kilifanya kazi kama hii katika malalo ya bibi Zainabu (a.s), matengenezo yaliyo fanywa katika malalo ya Huru bun Yazidi Riyahi (a.s) ni sehemu ya maandalizi ya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).