Miongoni mwa maandalizi ya ziara ya Arubaini: Idara ya mawasiliano ya Atabatu Abbasiyya tukufu yasambaza vibanda vya kutoa maelekezo na matangazo ya waliopotelewa..

Maoni katika picha
Vitengo mbalimbali vya Atabatu Abbasiyya tukufu vipo katika maandalizi makubwa ya ziara ya Arubainiyya ya Imamu Hussein (a.s), idara ya mawasiliano ni miongoni mwa idara zinazo fanya maandalizi mbalimbali, miongoni mwa maandalizi yake ni kuweka vibanda vya matangazo katika njia kuu zote zinazo ingia katika mji mtukufu wa Karbala upande wa Baabil, Najafu na Bagdad.

Uwekaji wa vibanda hivi unatokana na tatizo kubwa la kupotelewa na vitu au watu linalo wakuta mazuwaru (watu wanaokuja kufanya ziara) hususan kupotea kwa watoto katika ziara za mamilioni wa watu, pamoja na ziara hii ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), ambayo huzingatiwa kua ndio ziara kubwa zaidi, kwa hiyo vipanda hivi vimefunguliwa kwa ajili hiyo.

Kila kibanda kina:-

  • 1- Kila kibanda kina namba ya simu na mimu ya upepo (redio coll) pamoja na mtandao wa Intanet.
  • 2- Kompyuta iliyo onganishwa na program inayo iunganisha na kompyuta zote zilizopo katika vibanda hivi, ambapo kuna ukurasa wa kuandika maelezo na yakaonekana katika kompyuta zote.
  • 3- Kioo (Screen) kubwa inayo onyesha jina, umri na anuani ya aliye potea.
  • 4- Kipaza sauti kwa ajili ya matangazo ya walio potezana.
  • 5- Gari zinazo zungukia vibanda hivyo kwa ajili ya kupeleka watu watakao tambuliwa kwa wenzao au kuwapeleka katika kituo kikuu.
  • 6- Kitambulisho kitakacho andikwa jina la mtoto au mzee na namba ya simu, ili iwe rahisi kutambuliwa na kituo chochote.

Vibanda hivi vinafanya kazi kwa kushirikiana wao kwa wao samamba na kushirikiana pia na vibanda vilivyo wekwa na Atabatu Husseiniyya tukufu pamoja na vibanda vilivyopo katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu na vituo vikuu vya maelekezo na matangazo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: