Maukibu ya watumishi wa Ataba mbili tukufu wafanya taazia kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kumbukumbu ya kuuawa kwa ndugu yao Imamu Hassan (a.s)..

Maoni katika picha
Masikitiko yangu ni kwa Hassan mtakasifu, kwa yale aliyo fanyiwa na maadui, mtihani alio pata wa kupewa sumu kali, iliyo kata maini ya (mjukuu wa) Mtume, na kumhuzunisha kipenzi chake Zaharaa.

Watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, wamefanya kumbukumbu ya kuuawa kishahidi kwa mjukuu mkubwa wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ambaye ni Hassan Almujtaba (a.s), aliye uawa mwezi saba Safar, katika maukibu ya pamoja iliyo jumuisha viongozi na watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, wakiongozwa na katibu wao mkuu, Muhandisi Muhammad Ashiqar kwa ajili wa kufanya taazia kwa Imamu Hussein na Abulfadhil Abbasi (a.s) kutokana na msiba huo.

Baada ya kufanya taazia katika ukimbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), maukibu ikaelekea katika malalo ya Abuu Abdillahi Hussein (a.s), wakiwa wamebeba mfano wa jeneza la Imamu Hassan Almujtaba (a.s), wakapitia katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu, na kupokelewa na watumishi wa Atabatu Husseiniyya na wakafanya majlisi ya maombolezo ya pamoja katika ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s), katika majlisi hiyo zilisomwa kaswida mbalimbali zilizo elezea dhulma alizo fanyiwa Imamu (a.s) na mambo yaliyo jiri katika siku kama ya leo.

Pia katika ukumbi wa utawala ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu palifanyika majlisi ya maombolezo kwa ajili ya watumishi wake.

Kumbuka kua Ataba tukufu za Karbala hufanya maukibu ya kuadhimisha matukio mbalimbali, yakiwemo matukio ya kufariki kwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s) katika kipindi chote cha mwaka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: