Ewe bibi Allah akusaidie… karibu karibu Allah akuze malipo yako… na akulipe ewe ulotoka mbali, umekuja kutokea wapi… kutoka Basra una nini leo unatembea… umetembea siku sita na unataka kutembea hadi Karbala…anaweza kutembea kwa mapenzi ya Hussein.
(Nguvu haziji kwa uwezo wa mwili, bali kwa nguvu ya kiroho isiyo shindwa), umri wake ni zaidi ya miaka sabini hajazuiliwa na umri huo kutembea hadi Karbala, mzee huyu anatoa somo kwa watu waliopotea wasiojua haki za Ahlulbait (a.s), kwa nini isiwe hivyo na wewe ni miongoni mwa waliozaa majemedari imara na ukawanyonyesha maziwa yaliyo jaa mapenzi ya Hussein, na wakafuzu katika madrasa yako ewe mwenye subira.
Mgongo wako umepinda kutokana na ukubwa wa umri wako, moyo wako umejaa mapenzi ya Hussein haujali maradhi wala ukubwa wa umri wako, kila anaye kuona azma yake inaongezeka, na anafanya maamuzi ya kufika baada yako katika malalo ya bwana wa mashahidi na kuhuisha ziara ya Arubainiyya.
Wewe na wa mfano wako ni miongoni mwa wazee mnao mliwaza bibi Zaharaa, Zainabu na Ummul Banina, mnamtia nguvu kila aliye poteza mzazi wake, na nyie ndio wakina mama wa watu wanaokuja kumzuru Imamu Hussein, vipi mtu kama wewe unamapenzi makubwa kiasi hiki, na Mwenyezi Mungu kaiweka pepo chini ya nyayo zako.
Hakuna maneno ya kukuelezea ewe mama, na mimi naona Karbala imenyoosha mikono yake kukupokea, na wewe unakuja kufanya ibada ya ziara, kesho utapokelewa na Zaharaa ewe uleye mpa taazia.