Kufuatia ziara ya Arubaini: Mtandao wa kimataifa Alkafeel waboresha ukurasa wa picha ulio sanifiwa na kupangiliwa katika ubora mkubwa..

Maoni katika picha
Wataalamu wa mtandao wa kimataifa Alkafeel wameboresha ukurasa wa picha, ulio sanifiwa na kupangiliwa vizuri unao endana na maendeleo yaliyopo katika sekta hiyo.

Kwa mujibu wa maelezo ya Ustadh Haidari Mamitha kiongozi wa idara ya Intanet chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ambapo mtandao wa kimataifa wa Alkafeel ni miongoni mwa idara zake, amesema kua: “Tumeufanyia maboresho ukurasa wa picha, kutokana na malengo waliyo jiwekea idara ya Alkafeel ya kuboresha kurasa zao, na huu ni miongoni mwa kurasa muhimu katika mtandao”.

Akaongeza kusema kua: Maboresho yamehusisha vitu vingi, miongoni mwake ni:-

 • 1- Kuongeza kasi ya upekuzi.
 • 2- Urahisi wa kupakua.
 • 3- Unafanya kazi katika aina zote za upekuzi.
 • 4- Picha zipo katika muonekano boro unao bainisha kila kitu.
 • 5- Kuanzisha ukurasa unao toa fursa kwa wapiga picha kutuma picha zao na zinaweza kuingizwa katika mtandao baada ya kupasishwa.
 • 6- Kuboresha program ya utafutaji, kuanzia jina, ukubwa na tarehe.
 • 7- Sasa hivi kila mpiga picha anaweza kutengeneza ukurasa wake maalumu atakao tumia kutuma picha.
 • 8- Uwezekano wa kuweka maoni katika picha na kuweka pendeza (like).
 • 9- Urahisi wa kuhamisha picha baina ya kurasa.
 • 10- Urahisi wa kupekua picha na kuzipakua katika ubora mzuri anao hitaji mtazamaji.
 • 11- Kupangiliwa picha zinazo angaliwa zaidi na zinazo pakuliwa zaidi, pia kubainisha picha za zamani na mpya au kinyume chake.
 • 12- Kuanzisha alama ya utafutaji ambayo ni rahisi kuitumia.
 • 13- Kuongeza hash tak katika picha.
 • 14- Tumezingatia mipaka ya watumishi wa Intanet katika kufanya maboresho ya ukurasa huu.

Kwa kuangalia ukurasa huu na zingine unaweza kutumia anuani ifuatayo: https://alkafeel.net/photos/
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: