Vituo katika njia ya pepo: Mazuwaru kutoka katika Mkoa wa Waasit wakielekea Karbara..

Maoni katika picha
Zaidi ya siku mbili watu wa Waasit wanatembea kuelekea mkoa mtukufu wa Karbala kufanya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), chini ya maandalizi makubwa ya watoa huduma na ulinzi mkali kwa ajili ya kuhakikisha usalama wao.

Kwa mujibu wa kauli za viongozi wa eneo hilo, ndani ya siku mbili zijazo idadi ya mazuwaru itaongezeka mara dufu, hususan baada ya kuwasili sehemu kubwa ya mazuwaru wanaotoka katika mikoa ya kusini pamoja na watu wanao fatana nao kutoka nchi jirani ya Kuwait ambao hukutana katika eneo hilo.

Mazuwaru na mkoa wa Waasit na wale watakao ungana nao kutoka katika mikoa ya kusini na nchi jirani watatumia barabara kuu na ndogo kutoka Waasit wakipitia Nuumaniyya hadi Shahimiyya wanaenda hadi Shumliy katika mkoa wa Baabil kisha wanaenda hadi Karbala, kutoka makao makuu ya mkoa wa Waasit hadi kufika Karbala kuna umbali wa kilometa 180.

Mawakibu za kutoa huduma zimeenea njia yote, na wamejipanga imara kutoa huduma zote muhimu kwa mazuwaru, kama vile chakula, vinywaji, malazi, nguo pamoja na huduma za kitabibu na zinginezo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: