Imebaki wiki kufika siku ya ziara; Barabara zinazo elekea katika malalo za Karbala zafurika..

Maoni katika picha
Zimebaki siku saba kufika siku ya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), watu wanaokuja kufanya ziara wanaendelea kumiminika katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), huku barabara zote zinazo elekea katika mji wa kujitolea na shahada zikiwa zimefurika watu wanaokuja (Karbala) kutoka ndani na nje ya Iraq, inatarajiwa mwaka huu kutakua na idadi kubwa zaidi ya mazuwaru kushinda miaka iliyo pita.

Bado mikoa ya kusini inashuhudia misafara ya watu mfululizo wanao kwenda kufanya ziara ya Arubaini, baadhi yao ni kutoka katika mikoa hiyo na wengine wanatoka sehemu zingine, misafara imesha anza kuwasili Karbala na kila siku idadi ya misafara inayo wasili inaendelea kuongezeka, barabara zote zinazo ingia katika mji mtukufu wa Karbala zimejaa watu, huku mazingira yao yakisema; Eee! Bwana wangu, ewe Imamu wa zama Mwenyezi Mungu akuze malipo yako na atulize roho yako kwa kudhihiri kwako na kulipa kisasi cha babu yako Hussein (a.s) na sisi ni miongoni mwa watakao kunusuru na kukusaidia, tukubalie ewe Mola wa walimwengu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: