Atabatu Abbasiyya tukufu yaongeza sehemu za kutolea huduma kwa mazuwaru wa Arubaini..

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu inatumia nguvu zake zote za mali na watu kuhakikisha inatoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru, na kuwapunguzia uchovu wa safari, juhudi zao hazija ishia katika majengo yao peke yake, bali wamepanua wigo hadi katika shule na husseiniyya, wanafanya kazi ya kuandaa na kunufaika na eneo lote la uwanja wake.

Kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimewasiliana na uongozi wa mkoa wa Karbala na kupewa shule 12, wametumia fursa ya kusimama kwa masomo katika kipindi hiki, wanatoa madawati na kufanya usafi kisha wanatandika pamoja na kutoa huduma za chakula, maji na vinginevyo, wamechagua shule zilizopo katika maeneo yanye msongamano mkubwa wa mazuwaru na uchache wa mawakibu zinazo toa huduma za malazi kwa mazuwaru.

Kwa upande mwingine, kitengo cha utumishi kimeandaa Husseiniyya mbili karibu na haram mbili (Husseiniyya na Abbasiyya) tukufu, ambazo ni Husseiniyyatul Isfahaniyya na Husseiniyyatu Imamu Khuiy (r.a) na wameweka huduma zote kama walizo weka katika maeneo ya shule.

Pia kimepanga watumishi wake wanaofanya kazi kwa kushirikiana na watoa huduma wa kujitolea kwa ajili ya kusimamia shughuli zote zinazo endelea katika maeneo hayo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: