Mgahawa (mudhifu) wa Abulfadhil Abbasi wagawa zaidi ya sahani elfu 45 za chakula kila siku kwa mazuwaru wa Arubaini..

Maoni katika picha
Muendelezo wa wema na ukarimu wa mwenye malalo tukufu, na muendelezo wa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika kuwahudumia mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), unaotokana na imani yao kua; utukufu wa kumtumikia Zaharaa ndio mkubwa zaidi, watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wanafanya kila aina ya juhudi katika kuwatumikia mazuwaru hususan kitengo cha mgahawa (mudhifu) wa Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kutokana na ukarimu wao tumepata maneno murua kutoka kwa kiongozi wa kitengo cha mgahawa wa Abulfadhil Abbasi (a.s) Haji Kadhim Abdulhussein amesema: “Tumejifunza kutokana na majeraha ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kufanya kila tuwezalo kwa ajili ya kuhudumia mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)”. Maneno haya yanaonyesha utiifu wao kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na mapenzi yao kwa Hussein na ukarimu wao kwa Abbasi (a.s), hii ni bishara njema ya mustaqbali mzuri, juhuhudi hizi zimezaa matunda kwa watumishi wa mgahawa wa Abulfadhil Abbasi (a.s) ambao hufanya kazi usiku na mchana bila kupumzika, hasa katika siku za ziara, hutoa huduma ya kupokea wageni na kuwapa chakula masaa 24 kila siku, hadi sasa wanagawa zaidi ya sahani elfu 45 za chakula kwa siku, katika milo mitatu mikuu, ugawaji wa chakula hufanyika katika ukumbi wa mgahawa au kupitia madirisha ya nje yapatayo sita yaliyo tengwa kwa kazi hiyo (ya kugawa chakula).

Haji Kadhim akaongeza kusema kua: “Tulianza kujiandaa mapema kwa ajili ya ziara hii, na tukaandaa chakula cha kutosha katika vituo vyote vya mgahawa wa Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na matunda kwa ajili ya kugawa ndani ya mgahawa au katika maeneo ya nje”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: