Wahudumu wa mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s) wanashindana kutoa huduma za kila aina…

Maoni katika picha
Kila msimu wa ziara ya Arubaini, hushuhudiwa aina mbalimbali za utoaji wa huduma katika mawakibu zilizo enea njia nzima, kwa ajili ya kutoa huduma kwa mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s), kila mmoja hutoa huduma anazo penda.

Miongoni mwa huduma zinazo tolewa ni kutengeneza mikokoteni ya watoto na wakubwa, kituo hicho kinafanya kazi ya kurekebisha mikokoteni ya aina zote iliyo haribika kutokana na urefu wa safari.

Mmiliki wa kituo hicho, Bwana Juma Jabaar Shaibiy anaye ishi katika kitongoji cha (Shanafiyya) mkoani Diwaniyya amesema kua: “Kituo hiki kilianzishwa tangu miaka (6) iliyo pita, tunatengeneza mikokoteni ya wakubwa na watoto inayo milikuwa na mazuwaru wanao kwenda kufunya ziara ya Arubaini kwa kutembea hadi kwa Imamu Hussein (a.s)”.

Akaongeza kua: “Hua tunanunua spea na vifaa muhimu kwa kutumia pesa zetu binasfi kwa muda wa mwaka mzima, ili kuja kuvitumia kutengenezea mikokoteni ya mazuwaru watukufu wanao kwenda Karbala, tunatengeneza bure kati ya mikokoteni (400 – 500) kila siku”.

Akabainisha kua: “Mwaka huu tulianza kazi mapema sana kutokana na kuanza mapema kupita misafara ya mazuwaru wanao kwenda Karbala ya Hussein (a.s)”.

Bwana Juma akamalizia kwa kusema: “Tunamuomba Mwenyezi Mungu atukubalie hiki kidogo, kutokana na kazi hii tunatarajia kupata shifaa ya mwenye kumbukumbu hii siku ya kiyama na nimatumaini yetu kazi hii itaandikwa katika daftari la matendo yetu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: