Muda wa kuwasili kwa mawakibu za maombolezo (matam)…

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu husseiniyya za Iraq na ulimwengu wa kiislamu chini ya Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) wametoa ratiba inayo onyesha muda wa kuwasili kwa mawakibu za maombolezo (matam) katika tukio la ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) ya mwaka 1439 hijiriyya.

Kimetoa wito kwa viongozi wa mawakibu kuheshimu muda uliopangwa, hivyo kila maukibu itakua imepata nafasi mbili, nafasi ya kwanza maukibu ya (zanjiil) na ya pili ya (matam) kutokana na mkoa wake, na wanatakiwa wasihalifu mtiririko ulio pangwa na kubainishwa kwa watoa huduma wa Imamu Hussein (a.s) na mazuwaru wake watukufu.

18 Safar 1439h:

  • 1- Mkoa wa Dhiqaar wilaya na vitongoji vyake, kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 3 asubuhi.
  • 2- Mkoa wa Misaan wilaya na vitongoji vyake, kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 5 asubuhi.
  • 3- Maukibu ya kamati kuu na kikosi cha Badru, kuanzia saa 7 Adhuhuri hadi saa 8 mchana.
  • 4- Mikoa miwili ya Diyala na Swalahu-Dini, kuanzia saa 8 mchana hadi saa 10 Alasiri.
  • 5- Kikundi cha Answaaru wa Shahiid Swadri, kuanzia saa 10 Alasiri hadi saa 11:30 jioni.
  • 6- Mkoa wa Waasit wilaya na vitongoji vyake, kuanzia saa 12:30 jioni hadi saa 2 usiku.
  • 7- Mkoa wa Diwaniyya wilaya na vitongoji vyake, kuanzia saa 2 usiku hadi saa 4 usiku.
  • 8- Mkoa wa Bagdad wilaya na vitongoji vyake, kuanzia saa 4 usiku hadi saa 5 usiku.
  • 9- Mawakibu za nchi za kiarabu na kiislamu, kuanzia saa 5 usiku hadi saa 6 usiku.

19 Safar 1439h:

  • 1- Kadhimiyya tukufu, kuanzia saa 1 Asubuhi hadi saa 2 Asubuhi.
  • 2- Mkoa wa Najafu wilaya na vitongoji vyake, kuanzia saa 1 Asubuhi hadi saa 2 Asubuhi.
  • 3- Mkoa wa Basra wilaya na vitongoji vyake, kuanzia saa 3 Asubuhi hadi saa 5 Asubuhi.
  • 4- Mkoa wa Muthanah wilaya na vitongoji vyake, kuanzia saa 7 baada ya Adhuhuri hadi saa 8 baada ya Adhuhuri.
  • 5- Maukibu ya Hizbu Da’awah na kabila la Baniy Tamim, kuanzia saa 8 baada ya Adhuhuri hadi saa 9 Alasiri.
  • 6- Mkoa wa Baabil wilaya na vitongoji vyake, kuanzia saa 10 Alasiri hadi saa 11:30 jioni.
  • 7- Mkoa wa Karkuk na Nainawa, kuanzia saa 10 jioni hadi saa 3 usiku.
  • 8- Wilaya ya Ainu-Tamru, kuanzia saa 1 usiku hadi saa 3 usiku.
  • 9- Mawakibu za nchi za kiarabu na kiislamu, kuanzia saa 4 usiku hadi saa 6 usiku.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: