Kwa umakini na uangalifu mkubwa: Mtambo wa kuhesabu wa kielektronik unaendelea kuhesabu mazuwaru katika Atabatu Abbasiyya tukufu mwaka wa pili mfululizo…

Maoni katika picha
Uhesabuji wa watu wanaokuja kufanya ziara ya Arubaini ya mwaka 1439 Hijiriyya, unaendelea kwa mwaka wa pili mfululizo, mtambo wa kuhesabu watu chini ya idara ya mawasiliano katika Atabatu Abbasiyya tukufu, unaendelea kuhesabu watu wanao ingia katika mji mtukufu wa Karbala kupitia njia kuu tatu, (Bagdad – Karbala, Najafu – Karbala na Baabil – Karbala) pamoja na wale wanao ingia katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ispokua watu wanao tokea wilaya ya Husseiniyya na barabara ya Karbala – Ainu-Tamru.

Kufuatia swala hilo, mkuu wa idara ya mawasiliano chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Faras Abbasi Hamza amesema kua: “Mradi huu unahesabu watembea kwa miguu na waliopanda katika magari, tunatumia mitambo 12 ya kielektronik, inaingiza maelezo ya zaairi (mtu), urefu na unene, kama yupo ndani ya gari pia inaingiza maelezo ya gari, ukubwa na spidi yake, mitambo hiyo inafanya kazi saa 24 usiku na mchana, ilianza kuhesabu mwezi 7 Safar 1439h”.

Akasema kua: “Hadi kufikia mwezi 17 Safar 1439h, idadi jumla ya mazuwaru imefika (10,139,437)”.

Mkuu wa kituo cha taaluma na utafiti chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu Ustadh Jasaam Muhammad Saidi amesema kua: “Hakika kituo chetu kwa kushirikiana na idara ya mawasiliano katika Atabatu Abbasiyya tukufu, tutakamilisha taarifa rasmi ya ziara na itaambatanishwa na taarifa ya idadi inayo kusanywa na mitambo ya kielektronik pamoja na taarifa zingine zinazo kusanywa na vyombo vingine vya Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: