Mawakibu za matam zaanza kuhuisha Arubaini ya Imamu Hussein (a.s)..

Maoni katika picha
Asubuhi ya leo (18 Safar 1439h) sawa na (8 Novemba 2017m) mawakibu za matamu zimeanza kuomboleza msiba wa Imamu Hussein (a.s) katika ziara ya Arubaini.

Mawakibu hizi zimeanza maombolezo yao kwa kufuata ratiba iliyo pangwa na kitengo cha mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya), kila moja ilikua na muimbaji mahiri wa Qaswida, aliye imba kwa sauti ya huzuni yaliyo jiri kwa Imamu Hussein (a.s) na kuamsha hisia za wapenzi wa Ahlulbait (a.s) wanao huisha tukio hili chungu.

Kila maukibu inaanzia katika mlango wa Kibla wa Imamu Hussein (a.s) wanaingia katika haram yake tukufu, halafu wanapitia katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu na wanaenda hadi katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wanaingia katika haram hiyo kupitia mlango wa Imamu Hussein (a.s), na wanamaliza kwa kutokea katika mlango wa Kibla wa Abalfadhil Abbasi (a.s).

Mawakibu za kuomboleza zimezoea kuhuisha tukio hili, zimetengwa siku maalumu za mawakibu za zanjiil na siku maalumu za mawakibu za matam, kuanzia asubuhi hadi jioni baada ya Magharibi na Isha.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: