Umataifa wa msimu wa Arubaini waonyeshwa na mawakibu za kuomboleza kutoka katika nchi za kiarabu na kiajemi…

Maoni katika picha
Karbala ewe Kaaba ya mapenzi na utekelezaji.

Mapenzi ya Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake na maswahaba wake wema amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yao.

Kuzitendea haki zile damu takatifu zilizo acha harufu nzuri katika jangwa la Nainawa..

Kutokana na vigezo viwili hivyo (mapenzi na utekelezaji) utaona makundi ya waumini kutoka mashariki na magharibi ya aridhi wakielekeza nyuso zao upande wa Kibla ya watu huru, pamoja na kutofautiana kwa rangi zao, mitazamo yao, nasaba zao na madhehebu zao, wote wanakuja kufanya ziara kwa Imamu Hussein (a.s) na kuhuisha kumbukumbu ya Arubainiyya, kutokana na ukweli kua jambo hili ni la kibinadamu, lina utukufu mkubwa na kuunganisha watu wa aina na tabaka zote bila ubaguzi.

Mwaka huu ziara ya Arubaini imeshuhudia ongezeko kubwa la washiriki, kuanzia watu walio kuja kufanya ziara na vikundi vya mawakibu za kuomboleza na za kutoa huduma zilizo enea katika barabara zote za Iraq, na kufanya ushiriki wa wairaq kua wa kipekee kabisa, pia mawakibu nyingi za kuomboleza ziliingizwa katika orodha rasmi ya mawakibu na kupewa nafasi maalumu kwa mawakibu zote za matam na zainjiil.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: