Maahadi ya Qur’an tukufu yashiriki kwa vituo (130) vya Qur’an katika mradi wa vituo vya Qur’an…

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’an tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya uislamu na ubinadamu katika Atabatu Abbasiyya pamoja na matawi yake yote, wameshiriki katika mradi wa vituo vya Qur’an tukufu katika ziara ya Arubaini, na imesambaza wasomi wake wa Qur’an kwa ajili ya kuhudumia mamilioni ya watu wanaokwenda kwa bwana wa mashahidi (a.s).

Maahadi tukufu imefungua vituo 130 katika njia zote zinazo elekea katika mji mtukufu wa Karbala ya Hussein (a.s), wamefaya hivyo katika kushiriki kwao kwenye mradi huu mtukufu unaosimamiwa na uongozi mkuu wa Qur’an chuni ya Ataba na Mazaru tukufu kwa kusaidiana na umoja wa jumuiya za Qur’an za Iraq, Maahadi ya Qur’an inaushiriki mkubwa katika mradi huu, kuanzia uandaaji wa vituo pamoja na kuweka wasomaji.

Vituo hivyo vina majukumu mengi, miongoni mwa majukumu yake ni:

  • 1- Kufundisha usomaji sahihi wa Qur’an hususan kisomo cha ndani ya swala za faradhi.
  • 2- Kujibu maswali na kutoa ufafanuzi kuhusu mambo ya Qur’an.
  • 3- Kufanya mahafali na kisomo cha Qur’an katika kila kitongoji chenye kituo.
  • 4- Kugawa folda zenye nyaraka zinazo elezea maswala yanayo husu ziara na Qur.an.

Mkuu wa maahadi ya Qur’an tukufu shekh Nasrawi aliuambia mtandao Alkafeel kua: “Hakika vituo vya Qur’an vilivyopo katika njia zinazo elekea Karbala, vinafundisha Qur’an tukufu hususan surat Fatihah na surat Tauhid pamoja na nyeradi za kwenye swala za wajibu kwa sababu ni muhimu sana, kwani ukamilifu wa swala unategemea mambo hayo”.

Akaongeza kua: “Hakika Maahadi pamoja na matawi yake wameweka vituo vingi katika barabara kuu zinazo elekea Karbala tukufu, miongoni mwa barabara hizo ni (Bagdad – Karbala, Baabil – Karbala na Najafu – Karbala) mradi huu unafanyika kwa mwaka wa pili mfululizo chini ya usimamizi wa uongozi mkuu wa tume ya Qur’an ulio undwa na Ataba na Mazaru tukufu”.

Akabainisha kua: “Mwaka huu kulikua na vituo karibu (400) vilivyo undwa na Ataba mbalimbali pamoja na Mazaru tukufu na muungano wa jumuiya za Qur’an tukufu za Iraq, miongoni mwa vituo hivyo (130) tu ndio viko chini ya Maahadi, vituo vyote vimefanya kazi ya kufundisha usomaji sahihi wa Qur’an na vimegawa vipeperushi vinavyo fundisha mambo yanayo husu Qur’an pamoja na kutoa zawadi kwa mazuwaru walio fundishwa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: