Kikosi cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu chaanza kufanya usafi katika mji mtukufu wa Karbala…

Maoni katika picha
Asubuhi ya Juma Mosi ya (21 Safar 1439h) sawa na (11 Novemba 2017m) kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeanza kufanya usafi katika mji mtukufu wa Karbala kufuatia kukamilika kwa ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).

Kiongozi wa idara ya usafi katika kitengo cha utumishi cha Atabatu Abbasiyya tukufu na msimamizi mkuu wa kazi hiyo Ustadhi Riyadh Khadhir Hassan ameuambia mtandao wa Alkafeel kua:

“Tumeanza zoezi kubwa la kufanya usafi katika mji mtukufu wa Karbala, kwa kusafisha barabara zote kubwa na ndogo pamoja na maeneo ya karibu na haram tukufu zikiwemo shule tulizo tumia kuhifadhi mazuwaru, tumegawa makundi ya watu (6 – 10) wanaofanya kazi kwa zamu asubuhi na jioni, lengo ni kuhakikisha mji unakua katika muonekano mzuri, kwa sababu Karbala inapokea maelfu ya mazuwaru kila siku kutoka katika nchi tofauti na wenye tabia tofauti, kikosi hiki kinafanya juhudi ya pekee katika kusafisha mji”.

Watu wa miji mingine wamesifu na kuishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kwa huduma nzuri inazo toa.

Fahamu kua Atabatu Abbasiyya tukufu ilifanya kazi kubwa ya usafi kabla ya kuanza kwa kipindi cha ziara ya Arubaini katika maeneo mbalimbali ndani ya mji mtukufu wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: